The Word,
Made Clear
Read the Bible free
Kiswahili · Mathayo

Mathayo 4

Nani, nini, kwa nini, lini, wapi na jinsi — utangulizi wa kitabu

Jinsi ya kutumia uchunguzi wa maneno ya Kigiriki

Huhitaji kujua kusoma Kigiriki ili kuanza. Gusa neno lililopigiwa mstari katika mstari wa Kigiriki au wa Kigiriki kilichoandikwa kwa herufi za Kilatini: yote mawili yanafungua ingizo lilelile. Data inapopatikana kwa uhakika, utaona umbo la neno katika kamusi, sarufi, namba ya Strong na maana. Chagua “Zaidi kuhusu maana na sarufi” ili kuona maelezo zaidi. Buruta upau wa juu ili kusogeza paneli, na sogeza yaliyomo ndani yake ili kuendelea kusoma. Kitufe cha “Funga” hubaki kuonekana.

Mstari wa vipande unaonyesha kwamba uchanganuzi haupatikani; mstari maradufu unaonyesha kwamba ingizo la kamusi halipatikani. Hatujazii mapengo haya kwa kubahatisha. Kamusi hutoa maana zinazowezekana; muktadha huamua maana inayofaa katika kifungu. Maandishi yetu ya Biblia, Kigiriki na herufi za Kilatini hayajabadilishwa.

RASIMU KWA UHAKIKI: Maana za kamusi kwa Kiswahili ni tafsiri za kiotomatiki za ufafanuzi wa Kiingereza wa Dodson, pamoja na masahihisho maalumu. Bado zinahitaji uhakiki wa mwandishi na wa lugha. Ufafanuzi wa awali wa Kiingereza unapatikana katika maelezo yaliyopanuliwa. Alama hii ya rasimu inahusu maana za kamusi pekee, si maandishi yaliyokamilika ya Biblia.

Soma kuhusu vyanzo na upeo wa matumizi →
MATHAYO 4:1
TWMC · Kiswahili

Kisha Roho akamwongoza Yesu kwenda jangwani ili ajaribiwe na Ibilisi.

KJV · English

Then was Jesus led up of the Spirit into the wilderness to be tempted of the devil.

Kigiriki

Τότε ὁ Ἰησοῦς ἀνήχθη εἰς τὴν ἔρημον ὑπὸ τοῦ πνεύματος, πειρασθῆναι ὑπὸ τοῦ διαβόλου.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Tote ho Iēsous anēchthē eis tēn erēmon hypo tou pneumatos, peirasthēnai hypo tou diabolou.

MATHAYO 4:2
TWMC · Kiswahili

Baada ya kufunga siku arobaini na usiku arobaini, aliona njaa.

KJV · English

And when he had fasted forty days and forty nights, he was afterward an hungred.

Kigiriki

Καὶ νηστεύσας ἡμέρας τεσσαράκοντα καὶ νύκτας τεσσαράκοντα, ὕστερον ἐπείνασεν.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Kai nēsteusas hēmeras tessarakonta kai nyktas tessarakonta, hysteron epeinasen.

MATHAYO 4:3
TWMC · Kiswahili

Mjaribu akamjia, akasema, “Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mikate.”

KJV · English

And when the tempter came to him, he said, If thou be the Son of God, command that these stones be made bread.

Kigiriki

Καὶ προσελθὼν αὐτῷ ὁ πειράζων εἶπεν, Εἰ υἱὸς εἶ τοῦ θεοῦ, εἰπὲ ἵνα οἱ λίθοι οὗτοι ἄρτοι γένωνται.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Kai proselthōn autō ho peirazōn eipen, Ei huios ei tou theou, eipe hina hoi lithoi houtoi artoi genōntai.

MATHAYO 4:4
TWMC · Kiswahili

Yesu akajibu, “Imeandikwa, ‘Mtu hataishi kwa mkate peke yake, bali kwa kila neno linalotoka katika kinywa cha Mungu.’”

KJV · English

But he answered and said, It is written, Man shall not live by bread alone, but by every word that proceedeth out of the mouth of God.

Kigiriki

Ὁ δὲ ἀποκριθεὶς εἶπεν, Γέγραπται, Οὐκ ἐπ’ ἄρτῳ μόνῳ ζήσεται ἄνθρωπος, ἀλλ’ ἐπὶ παντὶ ῥήματι ἐκπορευομένῳ διὰ στόματος θεοῦ.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Ho de apokritheis eipen, Gegraptai, Ouk ep’ artō monō zēsetai anthrōpos, all’ epi panti rhēmati ekporeuomenō dia stomatos theou.

MATHAYO 4:5
TWMC · Kiswahili

Ndipo Ibilisi akamchukua mpaka mji mtakatifu, akamsimamisha kwenye kinara cha hekalu,

KJV · English

Then the devil taketh him up into the holy city, and setteth him on a pinnacle of the temple,

Kigiriki

Τότε παραλαμβάνει αὐτὸν ὁ διάβολος εἰς τὴν ἁγίαν πόλιν, καὶ ἵστησιν αὐτὸν ἐπὶ τὸ πτερύγιον τοῦ ἱεροῦ,

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Tote paralambanei auton ho diabolos eis tēn hagian polin, kai histēsin auton epi to pterygion tou hierou,

MATHAYO 4:6
TWMC · Kiswahili

akamwambia, “Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, jitupe chini. Kwa maana imeandikwa:

‘Atawaagiza malaika zake kuhusu wewe,’

na,

‘Watakubeba mikononi mwao,

usije ukajikwaa mguu wako kwenye jiwe.’”

KJV · English

And saith unto him, If thou be the Son of God, cast thyself down: for it is written, He shall give his angels charge concerning thee: and in their hands they shall bear thee up, lest at any time thou dash thy foot against a stone.

Kigiriki

καὶ λέγει αὐτῷ, Εἰ υἱὸς εἶ τοῦ θεοῦ, βάλε σεαυτὸν κάτω∙ γέγραπται γὰρ ὅτι Τοῖς ἀγγέλοις αὐτοῦ ἐντελεῖται περὶ σοῦ∙ καί, Ἐπὶ χειρῶν ἀροῦσίν σε, μήποτε προσκόψῃς πρὸς λίθον τὸν πόδα σοῦ.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

kai legei autō, Ei huios ei tou theou, bale seauton katō; gegraptai gar hoti Tois angelois autou enteleitai peri sou; kai, Epi cheirōn arousin se, mēpote proskopsēs pros lithon ton poda sou.

MATHAYO 4:7
TWMC · Kiswahili

Yesu akamwambia, “Imeandikwa pia, ‘Usimjaribu Bwana Mungu wako.’”

KJV · English

Jesus said unto him, It is written again, Thou shalt not tempt the Lord thy God.

Kigiriki

Ἔφη αὐτῷ ὁ Ἰησοῦς, Πάλιν γέγραπται, Οὐκ ἐκπειράσεις κύριον τὸν θεόν σου.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Ephē autō ho Iēsous, Palin gegraptai, Ouk ekpeiraseis kyrion ton theon sou.

MATHAYO 4:8
TWMC · Kiswahili

Tena Ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu sana, akamwonyesha falme zote za ulimwengu na fahari yake.

KJV · English

Again, the devil taketh him up into an exceeding high mountain, and sheweth him all the kingdoms of the world, and the glory of them;

Kigiriki

Πάλιν παραλαμβάνει αὐτὸν ὁ διάβολος εἰς ὄρος ὑψηλὸν λίαν, καὶ δείκνυσιν αὐτῷ πάσας τὰς βασιλείας τοῦ κόσμου καὶ τὴν δόξαν αὐτῶν,

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Palin paralambanei auton ho diabolos eis oros hypsēlon lian, kai deiknysin autō pasas tas basileias tou kosmou kai tēn doxan autōn,

MATHAYO 4:9
TWMC · Kiswahili

Akamwambia, “Nitakupa haya yote ukisujudu na kuniabudu.”

KJV · English

And saith unto him, All these things will I give thee, if thou wilt fall down and worship me.

Kigiriki

καὶ λέγει αὐτῷ, Ταῦτα πάντα σοι δώσω, ἐὰν πεσὼν προσκυνήσῃς μοι.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

kai legei autō, Tauta panta soi dōsō, ean pesōn proskynēsēs moi.

MATHAYO 4:10
TWMC · Kiswahili

Ndipo Yesu akamwambia, “Nenda nyuma yangu, Shetani! Kwa maana imeandikwa, ‘Utamwabudu Bwana Mungu wako, nawe utamtumikia Yeye peke yake.’”

KJV · English

Then saith Jesus unto him, Get thee hence, Satan: for it is written, Thou shalt worship the Lord thy God, and him only shalt thou serve.

Kigiriki

Τότε λέγει αὐτῷ ὁ Ἰησοῦς, Ὕπαγε ὀπίσω μου, Σατανᾶ∙ γέγραπται γάρ, Κύριον τὸν θεόν σου προσκυνήσεις, καὶ αὐτῷ μόνῳ λατρεύσεις.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Tote legei autō ho Iēsous, Hypage opisō mou, Satana; gegraptai gar, Kyrion ton theon sou proskynēseis, kai autō monō latreuseis.

MATHAYO 4:11
TWMC · Kiswahili

Ndipo Ibilisi akamwacha, na malaika wakaja wakamtumikia.

KJV · English

Then the devil leaveth him, and, behold, angels came and ministered unto him.

Kigiriki

Τότε ἀφίησιν αὐτὸν ὁ διάβολος∙ καὶ ἰδού, ἄγγελοι προσῆλθον καὶ διηκόνουν αὐτῷ.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Tote aphiēsin auton ho diabolos; kai idou, angeloi prosēlthon kai diēkonoun autō.

MATHAYO 4:12
TWMC · Kiswahili

Yesu aliposikia kwamba Yohana alikuwa ametiwa mikononi mwa watawala, aliondoka kwenda Galilaya.

KJV · English

¶ Now when Jesus had heard that John was cast into prison, he departed into Galilee;

Kigiriki

Ἀκούσας δὲ ὁ Ἰησοῦς ὅτι Ἰωάννης παρεδόθη, ἀνεχώρησεν εἰς τὴν Γαλιλαίαν∙

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Akousas de ho Iēsous hoti Iōannēs paredothē, anechōrēsen eis tēn Galilaian;

MATHAYO 4:13
TWMC · Kiswahili

Akaondoka Nazareti na kuishi Kapernaumu, karibu na ziwa, katika maeneo ya Zabuloni na Naftali.

KJV · English

And leaving Nazareth, he came and dwelt in Capernaum, which is upon the sea coast, in the borders of Zabulon and Nephthalim:

Kigiriki

καὶ καταλιπὼν τὴν Ναζαρέτ, ἐλθὼν κατῴκησεν εἰς Καπερναοὺμ τὴν παραθαλασσίαν, ἐν ὁρίοις Ζαβουλὼν καὶ Νεφθαλείμ∙

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

kai katalipōn tēn Nazaret, elthōn katōkēsen eis Kapernaoum tēn parathalassian, en horiois Zaboulōn kai Nephthaleim;

MATHAYO 4:14
TWMC · Kiswahili

Hivyo yakatimia yaliyosemwa kupitia nabii Isaya:

KJV · English

That it might be fulfilled which was spoken by Esaias the prophet, saying,

Kigiriki

ἵνα πληρωθῇ τὸ ῥηθὲν διὰ Ἠσαΐου τοῦ προφήτου, λέγοντος,

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

hina plērōthē to rhēthen dia Ēsaiou tou prophētou, legontos,

MATHAYO 4:15
TWMC · Kiswahili

“Nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali,

njia ya kuelekea baharini,

ng'ambo ya Yordani,

Galilaya ya watu wa mataifa,

KJV · English

The land of Zabulon, and the land of Nephthalim, by the way of the sea, beyond Jordan, Galilee of the Gentiles;

Kigiriki

Γῆ Ζαβουλὼν καὶ γῆ Νεφθαλείμ, ὁδὸν θαλάσσης, πέραν τοῦ Ἰορδάνου, Γαλιλαία τῶν ἐθνῶν,

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Gē Zaboulōn kai gē Nephthaleim, hodon thalassēs, peran tou Iordanou, Galilaia tōn ethnōn,

MATHAYO 4:16
TWMC · Kiswahili

watu waliokaa gizani

wameona nuru kuu,

na wale waliokaa katika nchi

na kivuli cha mauti,

nuru imewazukia.”

KJV · English

The people which sat in darkness saw great light; and to them which sat in the region and shadow of death light is sprung up.

Kigiriki

ὁ λαὸς ὁ καθήμενος ἐν σκότει εἶδεν φῶς μέγα, καὶ τοῖς καθημένοις ἐν χώρᾳ καὶ σκιᾷ θανάτου, φῶς ἀνέτειλεν αὐτοῖς.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

ho laos ho kathēmenos en skotei eiden phōs mega, kai tois kathēmenois en chōra kai skia thanatou, phōs aneteilen autois.

MATHAYO 4:17
TWMC · Kiswahili

Tangu wakati huo Yesu alianza kuhubiri, akisema:

“Tubuni, kwa maana Ufalme wa mbinguni umekaribia.”

KJV · English

¶ From that time Jesus began to preach, and to say, Repent: for the kingdom of heaven is at hand.

Kigiriki

Ἀπὸ τότε ἤρξατο ὁ Ἰησοῦς κηρύσσειν καὶ λέγειν, Μετανοεῖτε∙ ἤγγικεν γὰρ ἡ βασιλεία τῶν οὐρανῶν.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Apo tote ērxato ho Iēsous kēryssein kai legein, Metanoeite; ēngiken gar hē basileia tōn ouranōn.

MATHAYO 4:18
TWMC · Kiswahili

Alipokuwa akitembea kando ya Ziwa la Galilaya, aliwaona ndugu wawili, Simoni aitwaye Petro na Andrea ndugu yake, wakitupa wavu ziwani, kwa maana walikuwa wavuvi.

KJV · English

¶ And Jesus, walking by the sea of Galilee, saw two brethren, Simon called Peter, and Andrew his brother, casting a net into the sea: for they were fishers.

Kigiriki

Περιπατῶν δὲ παρὰ τὴν θάλασσαν τῆς Γαλιλαίας εἶδεν δύο ἀδελφούς, Σίμωνα τὸν λεγόμενον Πέτρον, καὶ Ἀνδρέαν τὸν ἀδελφὸν αὐτοῦ, βάλλοντας ἀμφίβληστρον εἰς τὴν θάλασσαν∙ ἦσαν γὰρ ἁλιεῖς.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Peripatōn de para tēn thalassan tēs Galilaias eiden dyo adelphous, Simōna ton legomenon Petron, kai Andrean ton adelphon autou, ballontas amphiblēstron eis tēn thalassan; ēsan gar halieis.

MATHAYO 4:19
TWMC · Kiswahili

Akawaambia, “Njooni mnifuate, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu.”

KJV · English

And he saith unto them, Follow me, and I will make you fishers of men.

Kigiriki

Καὶ λέγει αὐτοῖς, Δεῦτε ὀπίσω μου, καὶ ποιήσω ὑμᾶς ἁλιεῖς ἀνθρώπων.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Kai legei autois, Deute opisō mou, kai poiēsō hymas halieis anthrōpōn.

MATHAYO 4:20
TWMC · Kiswahili

Mara wakaacha nyavu zao, wakamfuata.

KJV · English

And they straightway left their nets, and followed him.

Kigiriki

Οἱ δὲ εὐθέως ἀφέντες τὰ δίκτυα ἠκολούθησαν αὐτῷ.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Hoi de eutheōs aphentes ta diktya ēkolouthēsan autō.

MATHAYO 4:21
TWMC · Kiswahili

Alipoendelea mbele, aliwaona ndugu wengine wawili, Yakobo mwana wa Zebedayo na Yohana ndugu yake, ndani ya mashua pamoja na Zebedayo baba yao, wakitengeneza nyavu zao. Akawaita,

KJV · English

And going on from thence, he saw other two brethren, James the son of Zebedee, and John his brother, in a ship with Zebedee their father, mending their nets; and he called them.

Kigiriki

Καὶ προβὰς ἐκεῖθεν, εἶδεν ἄλλους δύο ἀδελφούς, Ἰάκωβον τὸν τοῦ Ζεβεδαίου καὶ Ἰωάννην τὸν ἀδελφὸν αὐτοῦ, ἐν τῷ πλοίῳ μετὰ Ζεβεδαίου τοῦ πατρὸς αὐτῶν, καταρτίζοντας τὰ δίκτυα αὐτῶν∙ καὶ ἐκάλεσεν αὐτούς.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Kai probas ekeithen, eiden allous dyo adelphous, Iakōbon ton tou Zebedaiou kai Iōannēn ton adelphon autou, en tō ploiō meta Zebedaiou tou patros autōn, katartizontas ta diktya autōn; kai ekalesen autous.

MATHAYO 4:22
TWMC · Kiswahili

nao mara wakaacha mashua na baba yao, wakamfuata.

KJV · English

And they immediately left the ship and their father, and followed him.

Kigiriki

Οἱ δὲ εὐθέως ἀφέντες τὸ πλοῖον καὶ τὸν πατέρα αὐτῶν ἠκολούθησαν αὐτῷ.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Hoi de eutheōs aphentes to ploion kai ton patera autōn ēkolouthēsan autō.

MATHAYO 4:23
TWMC · Kiswahili

Yesu akazunguka Galilaya yote, akifundisha katika masinagogi yao, akitangaza Habari Njema ya Ufalme, na kuponya kila aina ya ugonjwa na udhaifu miongoni mwa watu.

KJV · English

¶ And Jesus went about all Galilee, teaching in their synagogues, and preaching the gospel of the kingdom, and healing all manner of sickness and all manner of disease among the people.

Kigiriki

Καὶ περιῆγεν ὅλην τὴν Γαλιλαίαν ὁ Ἰησοῦς, διδάσκων ἐν ταῖς συναγωγαῖς αὐτῶν, καὶ κηρύσσων τὸ εὐαγγέλιον τῆς βασιλείας, καὶ θεραπεύων πᾶσαν νόσον καὶ πᾶσαν μαλακίαν ἐν τῷ λαῷ.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Kai periēgen holēn tēn Galilaian ho Iēsous, didaskōn en tais synagōgais autōn, kai kēryssōn to euangelion tēs basileias, kai therapeuōn pasan noson kai pasan malakian en tō laō.

MATHAYO 4:24
TWMC · Kiswahili

Habari zake zikaenea Siria yote. Wakamletea wote waliokuwa wakiteseka kwa magonjwa mbalimbali na maumivu makali, waliokuwa wametawaliwa na pepo, waliopatwa na kifafa, na waliopooza; naye akawaponya.

KJV · English

And his fame went throughout all Syria: and they brought unto him all sick people that were taken with divers diseases and torments, and those which were possessed with devils, and those which were lunatick, and those that had the palsy; and he healed them.

Kigiriki

Καὶ ἀπῆλθεν ἡ ἀκοὴ αὐτοῦ εἰς ὅλην τὴν Συρίαν∙ καὶ προσήνεγκαν αὐτῷ πάντας τοὺς κακῶς ἔχοντας, ποικίλαις νόσοις καὶ βασάνοις συνεχομένους, καὶ δαιμονιζομένους, καὶ σεληνιαζομένους, καὶ παραλυτικούς∙ καὶ ἐθεράπευσεν αὐτούς.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Kai apēlthen hē akoē autou eis holēn tēn Syrian; kai prosēnenkan autō pantas tous kakōs echontas, poikilais nosois kai basanois synechomenous, kai daimonizomenous, kai selēniazomenous, kai paralytikous; kai etherapeusen autous.

MATHAYO 4:25
TWMC · Kiswahili

Makutano makubwa wakamfuata kutoka Galilaya, Dekapoli, Yerusalemu, Uyahudi, na ng'ambo ya Yordani.

KJV · English

And there followed him great multitudes of people from Galilee, and from Decapolis, and from Jerusalem, and from Judaea, and from beyond Jordan.

Kigiriki

Καὶ ἠκολούθησαν αὐτῷ ὄχλοι πολλοὶ ἀπὸ τῆς Γαλιλαίας καὶ Δεκαπόλεως καὶ Ἱεροσολύμων καὶ Ἰουδαίας καὶ πέραν τοῦ Ἰορδάνου.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Kai ēkolouthēsan autō ochloi polloi apo tēs Galilaias kai Dekapoleōs kai Hierosolymōn kai Ioudaias kai peran tou Iordanou.