Sura zote Vyanzo na toleo Kiswahili · Mathayo
Mathayo 28 Nani, nini, kwa nini, lini, wapi na jinsi — utangulizi wa kitabu
English · Español · Kiswahili Jinsi ya kutumia uchunguzi wa maneno ya Kigiriki Huhitaji kujua kusoma Kigiriki ili kuanza. Gusa neno lililopigiwa mstari katika mstari wa Kigiriki au wa Kigiriki kilichoandikwa kwa herufi za Kilatini: yote mawili yanafungua ingizo lilelile. Data inapopatikana kwa uhakika, utaona umbo la neno katika kamusi, sarufi, namba ya Strong na maana. Chagua “Zaidi kuhusu maana na sarufi” ili kuona maelezo zaidi. Buruta upau wa juu ili kusogeza paneli, na sogeza yaliyomo ndani yake ili kuendelea kusoma. Kitufe cha “Funga” hubaki kuonekana.
Mstari wa vipande unaonyesha kwamba uchanganuzi haupatikani; mstari maradufu unaonyesha kwamba ingizo la kamusi halipatikani. Hatujazii mapengo haya kwa kubahatisha. Kamusi hutoa maana zinazowezekana; muktadha huamua maana inayofaa katika kifungu. Maandishi yetu ya Biblia, Kigiriki na herufi za Kilatini hayajabadilishwa.
RASIMU KWA UHAKIKI: Maana za kamusi kwa Kiswahili ni tafsiri za kiotomatiki za ufafanuzi wa Kiingereza wa Dodson, pamoja na masahihisho maalumu. Bado zinahitaji uhakiki wa mwandishi na wa lugha. Ufafanuzi wa awali wa Kiingereza unapatikana katika maelezo yaliyopanuliwa. Alama hii ya rasimu inahusu maana za kamusi pekee, si maandishi yaliyokamilika ya Biblia.
Soma kuhusu vyanzo na upeo wa matumizi →
Washa JavaScript ili kutumia uchunguzi wa maneno. Sura Mathayo 1 Mathayo 2 Mathayo 3 Mathayo 4 Mathayo 5 Mathayo 6 Mathayo 7 Mathayo 8 Mathayo 9 Mathayo 10 Mathayo 11 Mathayo 12 Mathayo 13 Mathayo 14 Mathayo 15 Mathayo 16 Mathayo 17 Mathayo 18 Mathayo 19 Mathayo 20 Mathayo 21 Mathayo 22 Mathayo 23 Mathayo 24 Mathayo 25 Mathayo 26 Mathayo 27 Mathayo 28 Tafuta katika sura hii
MATHAYO 28:1 TWMC · Kiswahili
Baada ya Sabato, alfajiri ya siku ya kwanza ya juma ilipokuwa inaanza, Mariamu Magdalene na Mariamu yule mwingine walikuja kulitazama kaburi.
KJV · English
In the end of the sabbath, as it began to dawn toward the first day of the week, came Mary Magdalene and the other Mary to see the sepulchre.
Kigiriki
Ὀψὲ δὲ σαββάτων, τῇ ἐπιφωσκούσῃ εἰς μίαν σαββάτων, ἦλθεν Μαρία ἡ Μαγδαληνή, καὶ ἡ ἄλλη Μαρία, θεωρῆσαι τὸν τάφον.
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
Opse de sabbatōn, tē epiphōskousē eis mian sabbatōn, ēlthen Maria hē Magdalēnē, kai hē allē Maria, theōrēsai ton taphon.
MATHAYO 28:2 TWMC · Kiswahili
Tazama, tetemeko kubwa la ardhi likatokea, kwa maana malaika wa Bwana alishuka kutoka mbinguni, akaja kulivingirisha jiwe kutoka mlangoni na kuketi juu yake.
KJV · English
And, behold, there was a great earthquake: for the angel of the Lord descended from heaven, and came and rolled back the stone from the door, and sat upon it.
Kigiriki
Καὶ ἰδού, σεισμὸς ἐγένετο μέγας∙ ἄγγελος γὰρ κυρίου καταβὰς ἐξ οὐρανοῦ, προσελθὼν ἀπεκύλισεν τὸν λίθον ἀπὸ τῆς θύρας, καὶ ἐκάθητο ἐπάνω αὐτοῦ.
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
Kai idou, seismos egeneto megas; angelos gar kyriou katabas ex ouranou, proselthōn apekylisen ton lithon apo tēs thyras, kai ekathēto epanō autou.
MATHAYO 28:3 TWMC · Kiswahili
Mwonekano wake ulikuwa kama umeme, na mavazi yake meupe kama theluji.
KJV · English
His countenance was like lightning, and his raiment white as snow:
Kigiriki
Ἦν δὲ ἡ ἰδέα αὐτοῦ ὡς ἀστραπή, καὶ τὸ ἔνδυμα αὐτοῦ λευκὸν ὡσεὶ χιών.
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
Ēn de hē idea autou hōs astrapē, kai to endyma autou leukon hōsei chiōn.
MATHAYO 28:4 TWMC · Kiswahili
Walinzi wakatetemeka kwa kumwogopa, wakawa kama wafu.
KJV · English
And for fear of him the keepers did shake, and became as dead men .
Kigiriki
Ἀπὸ δὲ τοῦ φόβου αὐτοῦ ἐσείσθησαν οἱ τηροῦντες καὶ ἐγένοντο ὡσεὶ νεκροί.
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
Apo de tou phobou autou eseisthēsan hoi tērountes kai egenonto hōsei nekroi.
MATHAYO 28:5 TWMC · Kiswahili
Lakini malaika akawaambia wanawake, “Ninyi msiogope, kwa maana najua mnamtafuta Yesu aliyesulubiwa.
KJV · English
And the angel answered and said unto the women, Fear not ye: for I know that ye seek Jesus, which was crucified.
Kigiriki
Ἀποκριθεὶς δὲ ὁ ἄγγελος εἶπεν ταῖς γυναιξίν, Μὴ φοβεῖσθε ὑμεῖς∙ οἶδα γὰρ ὅτι Ἰησοῦν τὸν ἐσταυρωμένον ζητεῖτε.
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
Apokritheis de ho angelos eipen tais gynaixin, Mē phobeisthe hymeis; oida gar hoti Iēsoun ton estaurōmenon zēteite.
MATHAYO 28:6 TWMC · Kiswahili
Hayuko hapa, kwa maana amefufuka kama alivyosema! Njooni mwone mahali Bwana alipokuwa amelazwa.
KJV · English
He is not here: for he is risen, as he said. Come, see the place where the Lord lay.
Kigiriki
Οὐκ ἔστιν ὧδε∙ ἠγέρθη γάρ, καθὼς εἶπεν. Δεῦτε, ἴδετε τὸν τόπον ὅπου ἔκειτο ὁ κύριος.
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
Ouk estin hōde; ēgerthē gar, kathōs eipen. Deute, idete ton topon hopou ekeito ho kyrios.
MATHAYO 28:7 TWMC · Kiswahili
Nendeni haraka mkawaambie wanafunzi wake kwamba amefufuka kutoka kwa wafu. Tazameni, anawatangulia kwenda Galilaya; mtamwona huko.
Tazameni, nimewaambia.”
KJV · English
And go quickly, and tell his disciples that he is risen from the dead; and, behold, he goeth before you into Galilee; there shall ye see him: lo, I have told you.
Kigiriki
Καὶ ταχὺ πορευθεῖσαι εἴπατε τοῖς μαθηταῖς αὐτοῦ ὅτι Ἠγέρθη ἀπὸ τῶν νεκρῶν∙ καὶ ἰδού, προάγει ὑμᾶς εἰς τὴν Γαλιλαίαν∙ ἐκεῖ αὐτὸν ὄψεσθε∙ ἰδού, εἶπον ὑμῖν.
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
Kai tachy poreutheisai eipate tois mathētais autou hoti Ēgerthē apo tōn nekrōn; kai idou, proagei hymas eis tēn Galilaian; ekei auton opsesthe; idou, eipon hymin.
MATHAYO 28:8 TWMC · Kiswahili
Wakatoka haraka kaburini wakiwa na hofu na furaha kubwa, wakakimbia kuwaambia wanafunzi wake.
KJV · English
And they departed quickly from the sepulchre with fear and great joy; and did run to bring his disciples word.
Kigiriki
Καὶ ἐξελθοῦσαι ταχὺ ἀπὸ τοῦ μνημείου μετὰ φόβου καὶ χαρᾶς μεγάλης, ἔδραμον ἀπαγγεῖλαι τοῖς μαθηταῖς αὐτοῦ.
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
Kai exelthousai tachy apo tou mnēmeiou meta phobou kai charas megalēs, edramon apangeilai tois mathētais autou.
MATHAYO 28:9 TWMC · Kiswahili
Walipokuwa wakienda kuwaambia wanafunzi wake, tazama, Yesu akakutana nao,
akasema, “Furahini!”
Wakamjia, wakamshika miguu na kumwabudu.
KJV · English
¶ And as they went to tell his disciples, behold, Jesus met them, saying, All hail. And they came and held him by the feet, and worshipped him.
Kigiriki
Ὡς δὲ ἐπορεύοντο ἀπαγγεῖλαι τοῖς μαθηταῖς αὐτοῦ, καὶ ἰδού, Ἰησοῦς ἀπήντησεν αὐταῖς, λέγων, Χαίρετε. Αἱ δὲ προσελθοῦσαι ἐκράτησαν αὐτοῦ τοὺς πόδας, καὶ προσεκύνησαν αὐτῷ.
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
Hōs de eporeuonto apangeilai tois mathētais autou, kai idou, Iēsous apēntēsen autais, legōn, Chairete. Hai de proselthousai ekratēsan autou tous podas, kai prosekynēsan autō.
MATHAYO 28:10 TWMC · Kiswahili
Ndipo Yesu akawaambia, “Msiogope. Nendeni mkawaambie ndugu zangu waende Galilaya; huko wataniona.”
KJV · English
Then said Jesus unto them, Be not afraid: go tell my brethren that they go into Galilee, and there shall they see me.
Kigiriki
Τότε λέγει αὐταῖς ὁ Ἰησοῦς∙ Μὴ φοβεῖσθε∙ ὑπάγετε, ἀπαγγείλατε τοῖς ἀδελφοῖς μου ἵνα ἀπέλθωσιν εἰς τὴν Γαλιλαίαν, καὶ ἐκεῖ με ὄψονται.
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
Tote legei autais ho Iēsous; Mē phobeisthe; hypagete, apangeilate tois adelphois mou hina apelthōsin eis tēn Galilaian, kai ekei me opsontai.
MATHAYO 28:11 TWMC · Kiswahili
Walipokuwa njiani, baadhi ya walinzi wakaenda mjini, wakawajulisha makuhani wakuu kila kilichotokea.
KJV · English
¶ Now when they were going, behold, some of the watch came into the city, and shewed unto the chief priests all the things that were done.
Kigiriki
Πορευομένων δὲ αὐτῶν, ἰδού, τινὲς τῆς κουστωδίας ἐλθόντες εἰς τὴν πόλιν ἀπήγγειλαν τοῖς ἀρχιερεῦσιν ἅπαντα τὰ γενόμενα.
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
Poreuomenōn de autōn, idou, tines tēs koustōdias elthontes eis tēn polin apēngeilan tois archiereusin hapanta ta genomena.
MATHAYO 28:12 TWMC · Kiswahili
Makuhani wakuu wakakusanyika pamoja na wazee, wakashauriana, wakawapa askari fedha nyingi,
KJV · English
And when they were assembled with the elders, and had taken counsel, they gave large money unto the soldiers,
Kigiriki
Καὶ συναχθέντες μετὰ τῶν πρεσβυτέρων, συμβούλιόν τε λαβόντες, ἀργύρια ἱκανὰ ἔδωκαν τοῖς στρατιώταις,
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
Kai synachthentes meta tōn presbyterōn, symboulion te labontes, argyria hikana edōkan tois stratiōtais,
MATHAYO 28:13 TWMC · Kiswahili
wakisema, “Semeni, ‘Wanafunzi wake walikuja usiku, wakamwiba tulipokuwa tumelala.’
KJV · English
Saying, Say ye, His disciples came by night, and stole him away while we slept.
Kigiriki
λέγοντες, Εἴπατε ὅτι Οἱ μαθηταὶ αὐτοῦ νυκτὸς ἐλθόντες ἔκλεψαν αὐτὸν ἡμῶν κοιμωμένων.
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
legontes, Eipate hoti Hoi mathētai autou nyktos elthontes eklepsan auton hēmōn koimōmenōn.
MATHAYO 28:14 TWMC · Kiswahili
Jambo hili likifika masikioni mwa gavana, tutamshawishi na kuwaondolea matatizo.”
KJV · English
And if this come to the governor’s ears, we will persuade him, and secure you.
Kigiriki
Καὶ ἐὰν ἀκουσθῇ τοῦτο ἐπὶ τοῦ ἡγεμόνος, ἡμεῖς πείσομεν αὐτόν, καὶ ὑμᾶς ἀμερίμνους ποιήσομεν.
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
Kai ean akousthē touto epi tou hēgemonos, hēmeis peisomen auton, kai hymas amerimnous poiēsomen.
MATHAYO 28:15 TWMC · Kiswahili
Wakachukua fedha, wakafanya kama walivyofundishwa.
Na habari hii imeenea kati ya Wayahudi mpaka leo.
KJV · English
So they took the money, and did as they were taught: and this saying is commonly reported among the Jews until this day.
Kigiriki
Οἱ δὲ λαβόντες τὰ ἀργύρια ἐποίησαν ὡς ἐδιδάχθησαν. Καὶ διεφημίσθη ὁ λόγος οὗτος παρὰ Ἰουδαίοις μέχρι τῆς σήμερον.
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
Hoi de labontes ta argyria epoiēsan hōs edidachthēsan. Kai diephēmisthē ho logos houtos para Ioudaiois mechri tēs sēmeron.
MATHAYO 28:16 TWMC · Kiswahili
Wanafunzi kumi na mmoja wakaenda Galilaya, kwenye mlima ambao Yesu alikuwa amewaelekeza.
KJV · English
¶ Then the eleven disciples went away into Galilee, into a mountain where Jesus had appointed them.
Kigiriki
Οἱ δὲ ἕνδεκα μαθηταὶ ἐπορεύθησαν εἰς τὴν Γαλιλαίαν, εἰς τὸ ὄρος οὗ ἐτάξατο αὐτοῖς ὁ Ἰησοῦς.
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
Hoi de hendeka mathētai eporeuthēsan eis tēn Galilaian, eis to oros hou etaxato autois ho Iēsous.
MATHAYO 28:17 TWMC · Kiswahili
Walipomwona walimwabudu, lakini wengine wakasitasita.
KJV · English
And when they saw him, they worshipped him: but some doubted.
Kigiriki
Καὶ ἰδόντες αὐτὸν προσεκύνησαν αὐτῷ∙ οἱ δὲ ἐδίστασαν.
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
Kai idontes auton prosekynēsan autō; hoi de edistasan.
MATHAYO 28:18 TWMC · Kiswahili
Yesu akakaribia, akawaambia:
“Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.
KJV · English
And Jesus came and spake unto them, saying, All power is given unto me in heaven and in earth.
Kigiriki
Καὶ προσελθὼν ὁ Ἰησοῦς ἐλάλησεν αὐτοῖς, λέγων, Ἐδόθη μοι πᾶσα ἐξουσία ἐν οὐρανῷ καὶ ἐπὶ γῆς.
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
Kai proselthōn ho Iēsous elalēsen autois, legōn, Edothē moi pasa exousia en ouranō kai epi gēs.
MATHAYO 28:19 TWMC · Kiswahili
Nendeni mkawafanye watu wa mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu,
KJV · English
¶ Go ye therefore, and teach all nations, baptizing them in the name of the Father, and of the Son, and of the Holy Ghost:
Kigiriki
Πορευθέντες μαθητεύσατε πάντα τὰ ἔθνη, βαπτίζοντες αὐτοὺς εἰς τὸ ὄνομα τοῦ Πατρὸς καὶ τοῦ Υἱοῦ καὶ τοῦ Ἁγίου Πνεύματος∙
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
Poreuthentes mathēteusate panta ta ethnē, baptizontes autous eis to onoma tou Patros kai tou Huiou kai tou Hagiou Pneumatos;
MATHAYO 28:20 TWMC · Kiswahili
mkiwafundisha kushika yote niliyowaamuru.
Na tazameni, mimi niko pamoja nanyi siku zote, mpaka mwisho wa enzi hii.
Amina.”
KJV · English
Teaching them to observe all things whatsoever I have commanded you: and, lo, I am with you alway, even unto the end of the world. Amen.
Kigiriki
διδάσκοντες αὐτοὺς τηρεῖν πάντα ὅσα ἐνετειλάμην ὑμῖν∙ καὶ ἰδού, ἐγὼ μεθ’ ὑμῶν εἰμι πάσας τὰς ἡμέρας ἕως τῆς συντελείας τοῦ αἰῶνος. Ἀμήν.
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
didaskontes autous tērein panta hosa eneteilamēn hymin; kai idou, egō meth’ hymōn eimi pasas tas hēmeras heōs tēs synteleias tou aiōnos. Amēn.