The Word,
Made Clear
Read the Bible free
Kiswahili · Mathayo

Mathayo 10

Nani, nini, kwa nini, lini, wapi na jinsi — utangulizi wa kitabu

Jinsi ya kutumia uchunguzi wa maneno ya Kigiriki

Huhitaji kujua kusoma Kigiriki ili kuanza. Gusa neno lililopigiwa mstari katika mstari wa Kigiriki au wa Kigiriki kilichoandikwa kwa herufi za Kilatini: yote mawili yanafungua ingizo lilelile. Data inapopatikana kwa uhakika, utaona umbo la neno katika kamusi, sarufi, namba ya Strong na maana. Chagua “Zaidi kuhusu maana na sarufi” ili kuona maelezo zaidi. Buruta upau wa juu ili kusogeza paneli, na sogeza yaliyomo ndani yake ili kuendelea kusoma. Kitufe cha “Funga” hubaki kuonekana.

Mstari wa vipande unaonyesha kwamba uchanganuzi haupatikani; mstari maradufu unaonyesha kwamba ingizo la kamusi halipatikani. Hatujazii mapengo haya kwa kubahatisha. Kamusi hutoa maana zinazowezekana; muktadha huamua maana inayofaa katika kifungu. Maandishi yetu ya Biblia, Kigiriki na herufi za Kilatini hayajabadilishwa.

RASIMU KWA UHAKIKI: Maana za kamusi kwa Kiswahili ni tafsiri za kiotomatiki za ufafanuzi wa Kiingereza wa Dodson, pamoja na masahihisho maalumu. Bado zinahitaji uhakiki wa mwandishi na wa lugha. Ufafanuzi wa awali wa Kiingereza unapatikana katika maelezo yaliyopanuliwa. Alama hii ya rasimu inahusu maana za kamusi pekee, si maandishi yaliyokamilika ya Biblia.

Soma kuhusu vyanzo na upeo wa matumizi →
MATHAYO 10:1
TWMC · Kiswahili

Yesu akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa mamlaka juu ya roho wachafu ili wawafukuze, na mamlaka ya kuponya kila aina ya ugonjwa na udhaifu.

KJV · English

And when he had called unto him his twelve disciples, he gave them power against unclean spirits, to cast them out, and to heal all manner of sickness and all manner of disease.

Kigiriki

Καὶ προσκαλεσάμενος τοὺς δώδεκα μαθητὰς αὐτοῦ, ἔδωκεν αὐτοῖς ἐξουσίαν πνευμάτων ἀκαθάρτων, ὥστε ἐκβάλλειν αὐτά, καὶ θεραπεύειν πᾶσαν νόσον καὶ πᾶσαν μαλακίαν.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Kai proskalesamenos tous dōdeka mathētas autou, edōken autois exousian pneumatōn akathartōn, hōste ekballein auta, kai therapeuein pasan noson kai pasan malakian.

MATHAYO 10:2
TWMC · Kiswahili

Haya ndiyo majina ya mitume kumi na wawili:

Wa kwanza ni Simoni aitwaye Petro, na Andrea ndugu yake; Yakobo mwana wa Zebedayo, na Yohana ndugu yake;

KJV · English

Now the names of the twelve apostles are these; The first, Simon, who is called Peter, and Andrew his brother; James the son of Zebedee, and John his brother;

Kigiriki

Τῶν δὲ δώδεκα ἀποστόλων τὰ ὀνόματά ἐστιν ταῦτα∙ πρῶτος Σίμων ὁ λεγόμενος Πέτρος, καὶ Ἀνδρέας ὁ ἀδελφὸς αὐτοῦ∙ Ἰάκωβος ὁ τοῦ Ζεβεδαίου, καὶ Ἰωάννης ὁ ἀδελφὸς αὐτοῦ∙

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Tōn de dōdeka apostolōn ta onomata estin tauta; prōtos Simōn ho legomenos Petros, kai Andreas ho adelphos autou; Iakōbos ho tou Zebedaiou, kai Iōannēs ho adelphos autou;

MATHAYO 10:3
TWMC · Kiswahili

Filipo na Bartholomayo; Tomaso na Mathayo mtoza ushuru; Yakobo mwana wa Alfayo; na Lebayo, aliyeitwa pia Thadayo;

KJV · English

Philip, and Bartholomew; Thomas, and Matthew the publican; James the son of Alphaeus, and Lebbaeus, whose surname was Thaddaeus;

Kigiriki

Φίλιππος, καὶ Βαρθολομαῖος∙ Θωμᾶς, καὶ Ματθαῖος ὁ τελώνης∙ Ἰάκωβος ὁ τοῦ Ἀλφαίου, καὶ Λεββαῖος ὁ ἐπικληθεὶς Θαδδαῖος∙

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Philippos, kai Bartholomaios; Thōmas, kai Matthaios ho telōnēs; Iakōbos ho tou Alphaiou, kai Lebbaios ho epiklētheis Thaddaios;

MATHAYO 10:4
TWMC · Kiswahili

Simoni Mkananayo; na Yuda Iskariote, ambaye pia alimsaliti Yesu.

KJV · English

Simon the Canaanite, and Judas Iscariot, who also betrayed him.

Kigiriki

Σίμων ὁ Κανανίτης, καὶ Ἰούδας Ἰσκαριώτης ὁ καὶ παραδοὺς αὐτόν.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Simōn ho Kananitēs, kai Ioudas Iskariōtēs ho kai paradous auton.

MATHAYO 10:5
TWMC · Kiswahili

Yesu akawatuma hawa kumi na wawili, akiwaagiza hivi:

“Msiende kwenye njia ya watu wa mataifa, wala msiingie katika mji wa Wasamaria.

KJV · English

These twelve Jesus sent forth, and commanded them, saying, Go not into the way of the Gentiles, and into any city of the Samaritans enter ye not:

Kigiriki

Τούτους τοὺς δώδεκα ἀπέστειλεν ὁ Ἰησοῦς, παραγγείλας αὐτοῖς, λέγων, Εἰς ὁδὸν ἐθνῶν μὴ ἀπέλθητε, καὶ εἰς πόλιν Σαμαρειτῶν μὴ εἰσέλθητε∙

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Toutous tous dōdeka apesteilen ho Iēsous, parangeilas autois, legōn, Eis hodon ethnōn mē apelthēte, kai eis polin Samareitōn mē eiselthēte;

MATHAYO 10:6
TWMC · Kiswahili

Badala yake, waendeeni kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.

KJV · English

But go rather to the lost sheep of the house of Israel.

Kigiriki

πορεύεσθε δὲ μᾶλλον πρὸς τὰ πρόβατα τὰ ἀπολωλότα οἴκου Ἰσραήλ.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

poreuesthe de mallon pros ta probata ta apolōlota oikou Israēl.

MATHAYO 10:7
TWMC · Kiswahili

Mnapoenda, tangazeni ujumbe huu: ‘Ufalme wa mbinguni umekaribia.’

KJV · English

And as ye go, preach, saying, The kingdom of heaven is at hand.

Kigiriki

Πορευόμενοι δὲ κηρύσσετε, λέγοντες ὅτι Ἤγγικεν ἡ βασιλεία τῶν οὐρανῶν.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Poreuomenoi de kēryssete, legontes hoti Ēngiken hē basileia tōn ouranōn.

MATHAYO 10:8
TWMC · Kiswahili

Ponyeni wagonjwa, takaseni wenye ukoma, fukuzeni pepo. Mmepokea bure; toeni bure.

KJV · English

Heal the sick, cleanse the lepers, raise the dead, cast out devils: freely ye have received, freely give.

Kigiriki

Ἀσθενοῦντας θεραπεύετε, λεπροὺς καθαρίζετε, δαιμόνια ἐκβάλλετε∙ δωρεὰν ἐλάβετε, δωρεὰν δότε.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Asthenountas therapeuete, leprous katharizete, daimonia ekballete; dōrean elabete, dōrean dote.

MATHAYO 10:9
TWMC · Kiswahili

Msijipatie dhahabu, fedha, wala sarafu za shaba za kubeba katika mikanda yenu.

KJV · English

Provide neither gold, nor silver, nor brass in your purses,

Kigiriki

Μὴ κτήσησθε χρυσόν, μηδὲ ἄργυρον, μηδὲ χαλκὸν εἰς τὰς ζώνας ὑμῶν,

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Mē ktēsēsthe chryson, mēde argyron, mēde chalkon eis tas zōnas hymōn,

MATHAYO 10:10
TWMC · Kiswahili

Msichukue mfuko wa safari, kanzu ya ziada, viatu vya ziada, wala fimbo za ziada. Kwa maana mfanyakazi anastahili chakula chake.

KJV · English

Nor scrip for your journey, neither two coats, neither shoes, nor yet staves: for the workman is worthy of his meat.

Kigiriki

μὴ πήραν εἰς ὁδόν, μηδὲ δύο χιτῶνας, μηδὲ ὑποδήματα, μηδὲ ῥάβδους∙ ἄξιος γὰρ ὁ ἐργάτης τῆς τροφῆς αὐτοῦ ἐστιν.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

mē pēran eis hodon, mēde dyo chitōnas, mēde hypodēmata, mēde rhabdous; axios gar ho ergatēs tēs trophēs autou estin.

MATHAYO 10:11
TWMC · Kiswahili

Mnapoingia katika mji au kijiji chochote, ulizeni ni nani humo anayestahili kuwapokea, nanyi mkae kwake mpaka mtakapoondoka.

KJV · English

And into whatsoever city or town ye shall enter, enquire who in it is worthy; and there abide till ye go thence.

Kigiriki

Εἰς ἣν δ’ ἂν πόλιν ἢ κώμην εἰσέλθητε, ἐξετάσατε τίς ἐν αὐτῇ ἄξιός ἐστιν∙ κἀκεῖ μείνατε, ἕως ἂν ἐξέλθητε.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Eis hēn d’ an polin ē kōmēn eiselthēte, exetasate tis en autē axios estin; kakei meinate, heōs an exelthēte.

MATHAYO 10:12
TWMC · Kiswahili

Mnapoingia nyumbani, wasalimuni watu wa nyumba hiyo.

KJV · English

And when ye come into an house, salute it.

Kigiriki

Εἰσερχόμενοι δὲ εἰς τὴν οἰκίαν, ἀσπάσασθε αὐτήν.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Eiserchomenoi de eis tēn oikian, aspasasthe autēn.

MATHAYO 10:13
TWMC · Kiswahili

Ikiwa nyumba hiyo inastahili, amani yenu na ikae juu yake. Ikiwa haistahili, amani yenu na iwarudie ninyi.

KJV · English

And if the house be worthy, let your peace come upon it: but if it be not worthy, let your peace return to you.

Kigiriki

Καὶ ἐὰν μὲν ᾖ ἡ οἰκία ἀξία, ἐλθέτω ἡ εἰρήνη ὑμῶν ἐπ’ αὐτήν∙ ἐὰν δὲ μὴ ᾖ ἀξία, ἡ εἰρήνη ὑμῶν πρὸς ὑμᾶς ἐπιστραφήτω.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Kai ean men ē hē oikia axia, elthetō hē eirēnē hymōn ep’ autēn; ean de mē ē axia, hē eirēnē hymōn pros hymas epistraphētō.

MATHAYO 10:14
TWMC · Kiswahili

Mtu asipowapokea wala kuyasikiliza maneno yenu, tokeni katika nyumba hiyo au mji huo, mkung'ute mavumbi ya miguu yenu.

KJV · English

And whosoever shall not receive you, nor hear your words, when ye depart out of that house or city, shake off the dust of your feet.

Kigiriki

Καὶ ὃς ἐὰν μὴ δέξηται ὑμᾶς μηδὲ ἀκούσῃ τοὺς λόγους ὑμῶν, ἐξερχόμενοι τῆς οἰκίας ἢ τῆς πόλεως ἐκείνης, ἐκτινάξατε τὸν κονιορτὸν τῶν ποδῶν ὑμῶν.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Kai hos ean mē dexētai hymas mēde akousē tous logous hymōn, exerchomenoi tēs oikias ē tēs poleōs ekeinēs, ektinaxate ton koniorton tōn podōn hymōn.

MATHAYO 10:15
TWMC · Kiswahili

Kwa kweli nawaambia: siku ya hukumu itavumilika zaidi kwa nchi ya Sodoma na Gomora kuliko kwa mji huo.

KJV · English

Verily I say unto you, It shall be more tolerable for the land of Sodom and Gomorrha in the day of judgment, than for that city.

Kigiriki

Ἀμὴν λέγω ὑμῖν, ἀνεκτότερον ἔσται γῇ Σοδόμων καὶ Γομόρρων ἐν ἡμέρᾳ κρίσεως, ἢ τῇ πόλει ἐκείνῃ.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Amēn legō hymin, anektoteron estai gē Sodomōn kai Gomorrōn en hēmera kriseōs, ē tē polei ekeinē.

MATHAYO 10:16
TWMC · Kiswahili

Tazameni, ninawatuma kama kondoo katikati ya mbwa mwitu. Basi iweni werevu kama nyoka na wasio na hila kama njiwa.

KJV · English

¶ Behold, I send you forth as sheep in the midst of wolves: be ye therefore wise as serpents, and harmless as doves.

Kigiriki

Ἰδού, ἐγὼ ἀποστέλλω ὑμᾶς ὡς πρόβατα ἐν μέσῳ λύκων∙ γίνεσθε οὖν φρόνιμοι ὡς οἱ ὄφεις, καὶ ἀκέραιοι ὡς αἱ περιστεραί.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Idou, egō apostellō hymas hōs probata en mesō lykōn; ginesthe oun phronimoi hōs hoi opheis, kai akeraioi hōs hai peristerai.

MATHAYO 10:17
TWMC · Kiswahili

Jihadharini na watu. Watawakabidhi kwenye mabaraza, na kuwapiga mijeledi katika masinagogi yao.

KJV · English

But beware of men: for they will deliver you up to the councils, and they will scourge you in their synagogues;

Kigiriki

Προσέχετε δὲ ἀπὸ τῶν ἀνθρώπων∙ παραδώσουσιν γὰρ ὑμᾶς εἰς συνέδρια, καὶ ἐν ταῖς συναγωγαῖς αὐτῶν μαστιγώσουσιν ὑμᾶς∙

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Prosechete de apo tōn anthrōpōn; paradōsousin gar hymas eis synedria, kai en tais synagōgais autōn mastigōsousin hymas;

MATHAYO 10:18
TWMC · Kiswahili

Nanyi mtapelekwa mbele ya watawala na wafalme kwa sababu yangu, ili muwe ushuhuda kwao na kwa watu wa mataifa.

KJV · English

And ye shall be brought before governors and kings for my sake, for a testimony against them and the Gentiles.

Kigiriki

καὶ ἐπὶ ἡγεμόνας δὲ καὶ βασιλεῖς ἀχθήσεσθε ἕνεκεν ἐμοῦ, εἰς μαρτύριον αὐτοῖς καὶ τοῖς ἔθνεσιν.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

kai epi hēgemonas de kai basileis achthēsesthe heneken emou, eis martyrion autois kai tois ethnesin.

MATHAYO 10:19
TWMC · Kiswahili

Watakapowakabidhi, msihangaike kwa wasiwasi kuhusu mtakavyosema au mtakachosema. Kwa maana mtapewa cha kusema saa ileile,

KJV · English

But when they deliver you up, take no thought how or what ye shall speak: for it shall be given you in that same hour what ye shall speak.

Kigiriki

Ὅταν δὲ παραδιδῶσιν ὑμᾶς, μὴ μεριμνήσητε πῶς ἢ τί λαλήσητε∙ δοθήσεται γὰρ ὑμῖν ἐν ἐκείνῃ τῇ ὥρᾳ τί λαλήσετε∙

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Hotan de paradidōsin hymas, mē merimnēsēte pōs ē ti lalēsēte; dothēsetai gar hymin en ekeinē tē hōra ti lalēsete;

MATHAYO 10:20
TWMC · Kiswahili

kwa sababu si ninyi mnaosema, bali Roho wa Baba yenu ndiye anayesema ndani yenu.

KJV · English

For it is not ye that speak, but the Spirit of your Father which speaketh in you.

Kigiriki

οὐ γὰρ ὑμεῖς ἐστὲ οἱ λαλοῦντες, ἀλλὰ τὸ πνεῦμα τοῦ πατρὸς ὑμῶν τὸ λαλοῦν ἐν ὑμῖν.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

ou gar hymeis este hoi lalountes, alla to pneuma tou patros hymōn to laloun en hymin.

MATHAYO 10:21
TWMC · Kiswahili

Ndugu atamkabidhi ndugu yake auawe, na baba atamkabidhi mtoto wake. Watoto watawaasi wazazi wao na kusababisha wauawe.

KJV · English

And the brother shall deliver up the brother to death, and the father the child: and the children shall rise up against their parents, and cause them to be put to death.

Kigiriki

Παραδώσει δὲ ἀδελφὸς ἀδελφὸν εἰς θάνατον, καὶ πατὴρ τέκνον∙ καὶ ἐπαναστήσονται τέκνα ἐπὶ γονεῖς, καὶ θανατώσουσιν αὐτούς.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Paradōsei de adelphos adelphon eis thanaton, kai patēr teknon; kai epanastēsontai tekna epi goneis, kai thanatōsousin autous.

MATHAYO 10:22
TWMC · Kiswahili

Nanyi mtachukiwa na wote kwa sababu ya jina langu. Lakini atakayevumilia mpaka mwisho ndiye atakayeokolewa.

KJV · English

And ye shall be hated of all men for my name’s sake: but he that endureth to the end shall be saved.

Kigiriki

Καὶ ἔσεσθε μισούμενοι ὑπὸ πάντων διὰ τὸ ὄνομά μου∙ ὁ δὲ ὑπομείνας εἰς τέλος, οὗτος σωθήσεται.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Kai esesthe misoumenoi hypo pantōn dia to onoma mou; ho de hypomeinas eis telos, houtos sōthēsetai.

MATHAYO 10:23
TWMC · Kiswahili

Watakapowatesa katika mji mmoja, kimbilieni mwingine. Kwa kweli nawaambia: hamtamaliza kuipitia miji ya Israeli kabla Mwana wa Adamu hajaja.

KJV · English

But when they persecute you in this city, flee ye into another: for verily I say unto you, Ye shall not have gone over the cities of Israel, till the Son of man be come.

Kigiriki

Ὅταν δὲ διώκωσιν ὑμᾶς ἐν τῇ πόλει ταύτῃ, φεύγετε εἰς τὴν ἄλλην∙ ἀμὴν γὰρ λέγω ὑμῖν, οὐ μὴ τελέσητε τὰς πόλεις τοῦ Ἰσραήλ, ἕως ἂν ἔλθῃ ὁ υἱὸς τοῦ ἀνθρώπου.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Hotan de diōkōsin hymas en tē polei tautē, pheugete eis tēn allēn; amēn gar legō hymin, ou mē telesēte tas poleis tou Israēl, heōs an elthē ho huios tou anthrōpou.

MATHAYO 10:24
TWMC · Kiswahili

Mwanafunzi si mkuu kuliko mwalimu wake, wala mtumishi si mkuu kuliko bwana wake.

KJV · English

The disciple is not above his master, nor the servant above his lord.

Kigiriki

Οὐκ ἔστιν μαθητὴς ὑπὲρ τὸν διδάσκαλον, οὐδὲ δοῦλος ὑπὲρ τὸν κύριον αὐτοῦ.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Ouk estin mathētēs hyper ton didaskalon, oude doulos hyper ton kyrion autou.

MATHAYO 10:25
TWMC · Kiswahili

Inamtosha mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake, na mtumishi kama bwana wake. Ikiwa wamemwita mwenye nyumba Beelzebuli, je, si zaidi sana watawatukana watu wa nyumba yake?

KJV · English

It is enough for the disciple that he be as his master, and the servant as his lord. If they have called the master of the house Beelzebub, how much more shall they call them of his household?

Kigiriki

Ἀρκετὸν τῷ μαθητῇ ἵνα γένηται ὡς ὁ διδάσκαλος αὐτοῦ, καὶ ὁ δοῦλος ὡς ὁ κύριος αὐτοῦ. Εἰ τὸν οἰκοδεσπότην Βεελζεβοὺλ ἐκάλεσαν, πόσῳ μᾶλλον τοὺς οἰκειακοὺς αὐτοῦ;

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Arketon tō mathētē hina genētai hōs ho didaskalos autou, kai ho doulos hōs ho kyrios autou. Ei ton oikodespotēn Beelzeboul ekalesan, posō mallon tous oikeiakous autou?

MATHAYO 10:26
TWMC · Kiswahili

Basi msiwaogope. Hakuna kilichofunikwa ambacho hakitafunuliwa, wala kilichofichwa ambacho hakitajulikana.

KJV · English

Fear them not therefore: for there is nothing covered, that shall not be revealed; and hid, that shall not be known.

Kigiriki

Μὴ οὖν φοβηθῆτε αὐτούς∙ οὐδὲν γάρ ἐστιν κεκαλυμμένον ὃ οὐκ ἀποκαλυφθήσεται, καὶ κρυπτὸν ὃ οὐ γνωσθήσεται.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Mē oun phobēthēte autous; ouden gar estin kekalymmenon ho ouk apokalyphthēsetai, kai krypton ho ou gnōsthēsetai.

MATHAYO 10:27
TWMC · Kiswahili

Ninayowaambia gizani, yasemeni nuruni. Mnayosikia yakisemwa masikioni mwenu, yatangazeni juu ya paa za nyumba.

KJV · English

What I tell you in darkness, that speak ye in light: and what ye hear in the ear, that preach ye upon the housetops.

Kigiriki

Ὃ λέγω ὑμῖν ἐν τῇ σκοτίᾳ, εἴπατε ἐν τῷ φωτί∙ καὶ ὃ εἰς τὸ οὖς ἀκούετε, κηρύξατε ἐπὶ τῶν δωμάτων.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Ho legō hymin en tē skotia, eipate en tō phōti; kai ho eis to ous akouete, kēryxate epi tōn dōmatōn.

MATHAYO 10:28
TWMC · Kiswahili

Msiwaogope wanaoua mwili lakini hawawezi kuua nafsi. Bali mwogopeni zaidi Yule anayeweza kuangamiza nafsi na mwili katika Jehanamu.

KJV · English

And fear not them which kill the body, but are not able to kill the soul: but rather fear him which is able to destroy both soul and body in hell.

Kigiriki

Καὶ μὴ φοβεῖσθε ἀπὸ τῶν ἀποκτενόντων τὸ σῶμα, τὴν δὲ ψυχὴν μὴ δυναμένων ἀποκτεῖναι∙ φοβήθητε δὲ μᾶλλον τὸν δυνάμενον καὶ τὴν ψυχὴν καὶ τὸ σῶμα ἀπολέσαι ἐν γεέννῃ.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Kai mē phobeisthe apo tōn apoktenontōn to sōma, tēn de psychēn mē dynamenōn apokteinai; phobēthēte de mallon ton dynamenon kai tēn psychēn kai to sōma apolesai en geennē.

MATHAYO 10:29
TWMC · Kiswahili

Je, shomoro wawili hawauzwi kwa sarafu ndogo? Lakini hakuna hata mmoja wao atakayeanguka chini bila Baba yenu.

KJV · English

Are not two sparrows sold for a farthing? and one of them shall not fall on the ground without your Father.

Kigiriki

Οὐχὶ δύο στρουθία ἀσσαρίου πωλεῖται; Καὶ ἓν ἐξ αὐτῶν οὐ πεσεῖται ἐπὶ τὴν γῆν ἄνευ τοῦ πατρὸς ὑμῶν∙

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Ouchi dyo strouthia assariou pōleitai? Kai hen ex autōn ou peseitai epi tēn gēn aneu tou patros hymōn;

MATHAYO 10:30
TWMC · Kiswahili

Hata nywele za vichwa vyenu zote zimehesabiwa.

KJV · English

But the very hairs of your head are all numbered.

Kigiriki

ὑμῶν δὲ καὶ αἱ τρίχες τῆς κεφαλῆς πᾶσαι ἠριθμημέναι εἰσίν.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

hymōn de kai hai triches tēs kephalēs pasai ērithmēmenai eisin.

MATHAYO 10:31
TWMC · Kiswahili

Basi msiogope. Ninyi ni wa thamani zaidi kuliko shomoro wengi.

KJV · English

Fear ye not therefore, ye are of more value than many sparrows.

Kigiriki

Μὴ οὖν φοβηθῆτε∙ πολλῶν στρουθίων διαφέρετε ὑμεῖς.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Mē oun phobēthēte; pollōn strouthiōn diapherete hymeis.

MATHAYO 10:32
TWMC · Kiswahili

Kwa hiyo kila atakayenikiri mbele ya watu, nami nitamkiri mbele ya Baba yangu aliye mbinguni.

KJV · English

Whosoever therefore shall confess me before men, him will I confess also before my Father which is in heaven.

Kigiriki

Πᾶς οὖν ὅστις ὁμολογήσει ἐν ἐμοὶ ἔμπροσθεν τῶν ἀνθρώπων, ὁμολογήσω κἀγὼ ἐν αὐτῷ ἔμπροσθεν τοῦ πατρός μου τοῦ ἐν οὐρανοῖς.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Pas oun hostis homologēsei en emoi emprosthen tōn anthrōpōn, homologēsō kagō en autō emprosthen tou patros mou tou en ouranois.

MATHAYO 10:33
TWMC · Kiswahili

Lakini yeyote atakayenikana mbele ya watu, nami nitamkana mbele ya Baba yangu aliye mbinguni.

KJV · English

But whosoever shall deny me before men, him will I also deny before my Father which is in heaven.

Kigiriki

Ὅστις δ’ ἂν ἀρνήσηταί με ἔμπροσθεν τῶν ἀνθρώπων, ἀρνήσομαι αὐτὸν κἀγὼ ἔμπροσθεν τοῦ πατρός μου τοῦ ἐν οὐρανοῖς.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Hostis d’ an arnēsētai me emprosthen tōn anthrōpōn, arnēsomai auton kagō emprosthen tou patros mou tou en ouranois.

MATHAYO 10:34
TWMC · Kiswahili

Msifikiri kwamba nimekuja kuleta amani duniani. Sikuja kuleta amani, bali upanga.

KJV · English

Think not that I am come to send peace on earth: I came not to send peace, but a sword.

Kigiriki

Μὴ νομίσητε ὅτι ἦλθον βαλεῖν εἰρήνην ἐπὶ τὴν γῆν∙ οὐκ ἦλθον βαλεῖν εἰρήνην, ἀλλὰ μάχαιραν.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Mē nomisēte hoti ēlthon balein eirēnēn epi tēn gēn; ouk ēlthon balein eirēnēn, alla machairan.

MATHAYO 10:35
TWMC · Kiswahili

Kwa maana nimekuja kumtenganisha mtu na baba yake, binti na mama yake, na mkwe na mama mkwe wake.

KJV · English

For I am come to set a man at variance against his father, and the daughter against her mother, and the daughter in law against her mother in law.

Kigiriki

Ἦλθον γὰρ διχάσαι ἄνθρωπον κατὰ τοῦ πατρὸς αὐτοῦ, καὶ θυγατέρα κατὰ τῆς μητρὸς αὐτῆς, καὶ νύμφην κατὰ τῆς πενθερᾶς αὐτῆς∙

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Ēlthon gar dichasai anthrōpon kata tou patros autou, kai thygatera kata tēs mētros autēs, kai nymphēn kata tēs pentheras autēs;

MATHAYO 10:36
TWMC · Kiswahili

Na adui za mtu watakuwa watu wa nyumbani kwake mwenyewe.

KJV · English

And a man’s foes shall be they of his own household.

Kigiriki

καὶ ἐχθροὶ τοῦ ἀνθρώπου οἱ οἰκειακοὶ αὐτοῦ.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

kai echthroi tou anthrōpou hoi oikeiakoi autou.

MATHAYO 10:37
TWMC · Kiswahili

Anayempenda baba au mama kuliko mimi hanistahili. Anayempenda mwana au binti kuliko mimi hanistahili.

KJV · English

He that loveth father or mother more than me is not worthy of me: and he that loveth son or daughter more than me is not worthy of me.

Kigiriki

Ὁ φιλῶν πατέρα ἢ μητέρα ὑπὲρ ἐμέ, οὐκ ἔστιν μου ἄξιος∙ καὶ ὁ φιλῶν υἱὸν ἢ θυγατέρα ὑπὲρ ἐμέ, οὐκ ἔστιν μου ἄξιος∙

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Ho philōn patera ē mētera hyper eme, ouk estin mou axios; kai ho philōn huion ē thygatera hyper eme, ouk estin mou axios;

MATHAYO 10:38
TWMC · Kiswahili

Na asiyebeba msalaba wake na kunifuata hanistahili.

KJV · English

And he that taketh not his cross, and followeth after me, is not worthy of me.

Kigiriki

καὶ ὃς οὐ λαμβάνει τὸν σταυρὸν αὐτοῦ καὶ ἀκολουθεῖ ὀπίσω μου, οὐκ ἔστιν μου ἄξιος.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

kai hos ou lambanei ton stauron autou kai akolouthei opisō mou, ouk estin mou axios.

MATHAYO 10:39
TWMC · Kiswahili

Anayeyashikilia maisha yake atayapoteza, na anayepoteza maisha yake kwa sababu yangu atayapata.

KJV · English

He that findeth his life shall lose it: and he that loseth his life for my sake shall find it.

Kigiriki

Ὁ εὑρὼν τὴν ψυχὴν αὐτοῦ ἀπολέσει αὐτήν∙ καὶ ὁ ἀπολέσας τὴν ψυχὴν αὐτοῦ ἕνεκεν ἐμοῦ εὑρήσει αὐτήν.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Ho heurōn tēn psychēn autou apolesei autēn; kai ho apolesas tēn psychēn autou heneken emou heurēsei autēn.

MATHAYO 10:40
TWMC · Kiswahili

Anayewapokea ninyi ananipokea mimi, na anayenipokea mimi anampokea Yule aliyenituma.

KJV · English

¶ He that receiveth you receiveth me, and he that receiveth me receiveth him that sent me.

Kigiriki

Ὁ δεχόμενος ὑμᾶς ἐμὲ δέχεται∙ καὶ ὁ ἐμὲ δεχόμενος δέχεται τὸν ἀποστείλαντά με.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Ho dechomenos hymas eme dechetai; kai ho eme dechomenos dechetai ton aposteilanta me.

MATHAYO 10:41
TWMC · Kiswahili

Anayempokea nabii kwa sababu ni nabii atapokea thawabu ya nabii. Anayempokea mwenye haki kwa sababu ni mwenye haki atapokea thawabu ya mwenye haki.

KJV · English

He that receiveth a prophet in the name of a prophet shall receive a prophet’s reward; and he that receiveth a righteous man in the name of a righteous man shall receive a righteous man’s reward.

Kigiriki

Ὁ δεχόμενος προφήτην εἰς ὄνομα προφήτου μισθὸν προφήτου λήψεται∙ καὶ ὁ δεχόμενος δίκαιον εἰς ὄνομα δικαίου μισθὸν δικαίου λήψεται.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Ho dechomenos prophētēn eis onoma prophētou misthon prophētou lēpsetai; kai ho dechomenos dikaion eis onoma dikaiou misthon dikaiou lēpsetai.

MATHAYO 10:42
TWMC · Kiswahili

Na yeyote atakayempa hata kikombe cha maji baridi mmoja wa hawa wadogo kwa sababu ni mwanafunzi wangu—kwa kweli nawaambia, mtu huyo hatapoteza thawabu yake kamwe.”

KJV · English

And whosoever shall give to drink unto one of these little ones a cup of cold water only in the name of a disciple, verily I say unto you, he shall in no wise lose his reward.

Kigiriki

Καὶ ὃς ἐὰν ποτίσῃ ἕνα τῶν μικρῶν τούτων ποτήριον ψυχροῦ μόνον εἰς ὄνομα μαθητοῦ, ἀμὴν λέγω ὑμῖν, οὐ μὴ ἀπολέσῃ τὸν μισθὸν αὐτοῦ.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Kai hos ean potisē hena tōn mikrōn toutōn potērion psychrou monon eis onoma mathētou, amēn legō hymin, ou mē apolesē ton misthon autou.