Sura zote Vyanzo na toleo Kiswahili · Mathayo
Mathayo 18 Nani, nini, kwa nini, lini, wapi na jinsi — utangulizi wa kitabu
English · Español · Kiswahili Jinsi ya kutumia uchunguzi wa maneno ya Kigiriki Huhitaji kujua kusoma Kigiriki ili kuanza. Gusa neno lililopigiwa mstari katika mstari wa Kigiriki au wa Kigiriki kilichoandikwa kwa herufi za Kilatini: yote mawili yanafungua ingizo lilelile. Data inapopatikana kwa uhakika, utaona umbo la neno katika kamusi, sarufi, namba ya Strong na maana. Chagua “Zaidi kuhusu maana na sarufi” ili kuona maelezo zaidi. Buruta upau wa juu ili kusogeza paneli, na sogeza yaliyomo ndani yake ili kuendelea kusoma. Kitufe cha “Funga” hubaki kuonekana.
Mstari wa vipande unaonyesha kwamba uchanganuzi haupatikani; mstari maradufu unaonyesha kwamba ingizo la kamusi halipatikani. Hatujazii mapengo haya kwa kubahatisha. Kamusi hutoa maana zinazowezekana; muktadha huamua maana inayofaa katika kifungu. Maandishi yetu ya Biblia, Kigiriki na herufi za Kilatini hayajabadilishwa.
RASIMU KWA UHAKIKI: Maana za kamusi kwa Kiswahili ni tafsiri za kiotomatiki za ufafanuzi wa Kiingereza wa Dodson, pamoja na masahihisho maalumu. Bado zinahitaji uhakiki wa mwandishi na wa lugha. Ufafanuzi wa awali wa Kiingereza unapatikana katika maelezo yaliyopanuliwa. Alama hii ya rasimu inahusu maana za kamusi pekee, si maandishi yaliyokamilika ya Biblia.
Soma kuhusu vyanzo na upeo wa matumizi →
Washa JavaScript ili kutumia uchunguzi wa maneno. Sura Mathayo 1 Mathayo 2 Mathayo 3 Mathayo 4 Mathayo 5 Mathayo 6 Mathayo 7 Mathayo 8 Mathayo 9 Mathayo 10 Mathayo 11 Mathayo 12 Mathayo 13 Mathayo 14 Mathayo 15 Mathayo 16 Mathayo 17 Mathayo 18 Mathayo 19 Mathayo 20 Mathayo 21 Mathayo 22 Mathayo 23 Mathayo 24 Mathayo 25 Mathayo 26 Mathayo 27 Mathayo 28 Tafuta katika sura hii
MATHAYO 18:1 TWMC · Kiswahili
Wakati huo wanafunzi walimjia Yesu, wakamuuliza, “Basi ni nani aliye mkuu zaidi katika Ufalme wa mbinguni?”
KJV · English
At the same time came the disciples unto Jesus, saying, Who is the greatest in the kingdom of heaven?
Kigiriki
Ἐν ἐκείνῃ τῇ ὥρᾳ προσῆλθον οἱ μαθηταὶ τῷ Ἰησοῦ, λέγοντες, Τίς ἄρα μείζων ἐστὶν ἐν τῇ βασιλείᾳ τῶν οὐρανῶν;
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
En ekeinē tē hōra prosēlthon hoi mathētai tō Iēsou, legontes, Tis ara meizōn estin en tē basileia tōn ouranōn?
MATHAYO 18:2 TWMC · Kiswahili
Yesu akamwita mtoto mdogo, akamsimamisha katikati yao,
KJV · English
And Jesus called a little child unto him, and set him in the midst of them,
Kigiriki
Καὶ προσκαλεσάμενος ὁ Ἰησοῦς παιδίον ἔστησεν αὐτὸ ἐν μέσῳ αὐτῶν,
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
Kai proskalesamenos ho Iēsous paidion estēsen auto en mesō autōn,
MATHAYO 18:3 TWMC · Kiswahili
akasema, “Kwa kweli nawaambia, msipogeuka na kuwa kama watoto wadogo, hamtaingia kamwe katika Ufalme wa mbinguni.
KJV · English
And said, Verily I say unto you, Except ye be converted, and become as little children, ye shall not enter into the kingdom of heaven.
Kigiriki
καὶ εἶπεν, Ἀμὴν λέγω ὑμῖν, ἐὰν μὴ στραφῆτε καὶ γένησθε ὡς τὰ παιδία, οὐ μὴ εἰσέλθητε εἰς τὴν βασιλείαν τῶν οὐρανῶν.
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
kai eipen, Amēn legō hymin, ean mē straphēte kai genēsthe hōs ta paidia, ou mē eiselthēte eis tēn basileian tōn ouranōn.
MATHAYO 18:4 TWMC · Kiswahili
Basi yeyote anayejinyenyekeza kama mtoto huyu ndiye aliye mkuu zaidi katika Ufalme wa mbinguni.
KJV · English
Whosoever therefore shall humble himself as this little child, the same is greatest in the kingdom of heaven.
Kigiriki
Ὅστις οὖν ταπεινώσει ἑαυτὸν ὡς τὸ παιδίον τοῦτο, οὗτός ἐστιν ὁ μείζων ἐν τῇ βασιλείᾳ τῶν οὐρανῶν.
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
Hostis oun tapeinōsei heauton hōs to paidion touto, houtos estin ho meizōn en tē basileia tōn ouranōn.
MATHAYO 18:5 TWMC · Kiswahili
Na yeyote anayempokea mtoto mmoja kama huyu kwa jina langu ananipokea Mimi.
KJV · English
And whoso shall receive one such little child in my name receiveth me.
Kigiriki
Καὶ ὃς ἐὰν δέξηται παιδίον τοιοῦτον ἓν ἐπὶ τῷ ὀνόματί μου, ἐμὲ δέχεται∙
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
Kai hos ean dexētai paidion toiouton hen epi tō onomati mou, eme dechetai;
MATHAYO 18:6 TWMC · Kiswahili
Lakini yeyote anayemkwaza mmoja wa hawa wadogo wanaoniamini akaanguka dhambini, ingekuwa afadhali afungiwe jiwe kubwa la kusagia shingoni na azamishwe katika kilindi cha bahari.
KJV · English
But whoso shall offend one of these little ones which believe in me, it were better for him that a millstone were hanged about his neck, and that he were drowned in the depth of the sea.
Kigiriki
ὃς δ’ ἂν σκανδαλίσῃ ἕνα τῶν μικρῶν τούτων τῶν πιστευόντων εἰς ἐμέ, συμφέρει αὐτῷ ἵνα κρεμασθῇ μύλος ὀνικὸς εἰς τὸν τράχηλον αὐτοῦ, καὶ καταποντισθῇ ἐν τῷ πελάγει τῆς θαλάσσης.
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
hos d’ an skandalisē hena tōn mikrōn toutōn tōn pisteuontōn eis eme, sympherei autō hina kremasthē mylos onikos eis ton trachēlon autou, kai katapontisthē en tō pelagei tēs thalassēs.
MATHAYO 18:7 TWMC · Kiswahili
Ole kwa ulimwengu kwa sababu ya vikwazo vinavyowaangusha watu! Ni lazima vikwazo vije, lakini ole kwa mtu yule anayevileta!
KJV · English
¶ Woe unto the world because of offences! for it must needs be that offences come; but woe to that man by whom the offence cometh!
Kigiriki
Οὐαὶ τῷ κόσμῳ ἀπὸ τῶν σκανδάλων∙ ἀνάγκη γάρ ἐστιν ἐλθεῖν τὰ σκάνδαλα∙ πλὴν οὐαὶ τῷ ἀνθρώπῳ ἐκείνῳ, δι’ οὗ τὸ σκάνδαλον ἔρχεται.
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
Ouai tō kosmō apo tōn skandalōn; anankē gar estin elthein ta skandala; plēn ouai tō anthrōpō ekeinō, di’ hou to skandalon erchetai.
MATHAYO 18:8 TWMC · Kiswahili
Basi mkono wako au mguu wako ukikukwaza ukaanguka dhambini, ukate na kuutupa mbali nawe. Ni afadhali uingie uzimani ukiwa na ulemavu wa mguu au mkono kuliko kuwa na mikono miwili au miguu miwili na kutupwa katika moto wa milele.
KJV · English
Wherefore if thy hand or thy foot offend thee, cut them off, and cast them from thee: it is better for thee to enter into life halt or maimed, rather than having two hands or two feet to be cast into everlasting fire.
Kigiriki
Εἰ δὲ ἡ χείρ σου ἢ ὁ πούς σου σκανδαλίζει σε, ἔκκοψον αὐτὰ καὶ βάλε ἀπὸ σοῦ∙ καλόν σοι ἐστὶν εἰσελθεῖν εἰς τὴν ζωὴν χωλὸν ἢ κυλλόν, ἢ δύο χεῖρας ἢ δύο πόδας ἔχοντα βληθῆναι εἰς τὸ πῦρ τὸ αἰώνιον.
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
Ei de hē cheir sou ē ho pous sou skandalizei se, ekkopson auta kai bale apo sou; kalon soi estin eiselthein eis tēn zōēn chōlon ē kyllon, ē dyo cheiras ē dyo podas echonta blēthēnai eis to pyr to aiōnion.
MATHAYO 18:9 TWMC · Kiswahili
Jicho lako likikukwaza ukaanguka dhambini, ling'oe na kulitupa mbali nawe. Ni afadhali uingie uzimani ukiwa na jicho moja kuliko kuwa na macho mawili na kutupwa katika moto wa Jehanamu.
KJV · English
And if thine eye offend thee, pluck it out, and cast it from thee: it is better for thee to enter into life with one eye, rather than having two eyes to be cast into hell fire.
Kigiriki
Καὶ εἰ ὁ ὀφθαλμός σου σκανδαλίζει σε, ἔξελε αὐτὸν καὶ βάλε ἀπὸ σοῦ∙ καλόν σοι ἐστὶν μονόφθαλμον εἰς τὴν ζωὴν εἰσελθεῖν, ἢ δύο ὀφθαλμοὺς ἔχοντα βληθῆναι εἰς τὴν γέενναν τοῦ πυρός.
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
Kai ei ho ophthalmos sou skandalizei se, exele auton kai bale apo sou; kalon soi estin monophthalmon eis tēn zōēn eiselthein, ē dyo ophthalmous echonta blēthēnai eis tēn geennan tou pyros.
MATHAYO 18:10 TWMC · Kiswahili
Angalieni msimdharau hata mmoja wa hawa wadogo. Kwa maana nawaambia, malaika wao mbinguni huutazama daima uso wa Baba yangu aliye mbinguni.
KJV · English
Take heed that ye despise not one of these little ones; for I say unto you, That in heaven their angels do always behold the face of my Father which is in heaven.
Kigiriki
Ὁρᾶτε μὴ καταφρονήσητε ἑνὸς τῶν μικρῶν τούτων, λέγω γὰρ ὑμῖν ὅτι οἱ ἄγγελοι αὐτῶν ἐν οὐρανοῖς διὰ παντὸς βλέπουσιν τὸ πρόσωπον τοῦ πατρός μου τοῦ ἐν οὐρανοῖς.
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
Horate mē kataphronēsēte henos tōn mikrōn toutōn, legō gar hymin hoti hoi angeloi autōn en ouranois dia pantos blepousin to prosōpon tou patros mou tou en ouranois.
MATHAYO 18:11 TWMC · Kiswahili
Kwa maana Mwana wa Adamu alikuja kuokoa kilichopotea.
KJV · English
For the Son of man is come to save that which was lost.
Kigiriki
Ἦλθεν γὰρ ὁ υἱὸς τοῦ ἀνθρώπου σῶσαι τὸ ἀπολωλός.
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
Ēlthen gar ho huios tou anthrōpou sōsai to apolōlos.
MATHAYO 18:12 TWMC · Kiswahili
Mnaonaje? Mtu akiwa na kondoo mia moja, mmoja wao akapotea, je, hatawaacha wale tisini na tisa na kwenda milimani kumtafuta aliyepotea?
KJV · English
How think ye? if a man have an hundred sheep, and one of them be gone astray, doth he not leave the ninety and nine, and goeth into the mountains, and seeketh that which is gone astray?
Kigiriki
Τί ὑμῖν δοκεῖ; Ἐὰν γένηταί τινι ἀνθρώπῳ ἑκατὸν πρόβατα, καὶ πλανηθῇ ἓν ἐξ αὐτῶν∙ οὐχὶ ἀφεὶς τὰ ἐνενήκοντα ἐννέα, ἐπὶ τὰ ὄρη πορευθεὶς ζητεῖ τὸ πλανώμενον;
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
Ti hymin dokei? Ean genētai tini anthrōpō hekaton probata, kai planēthē hen ex autōn; ouchi apheis ta enenēkonta ennea, epi ta orē poreutheis zētei to planōmenon?
MATHAYO 18:13 TWMC · Kiswahili
Akimpata, kwa kweli nawaambia, anamfurahia huyo kuliko wale tisini na tisa ambao hawakupotea.
KJV · English
And if so be that he find it, verily I say unto you, he rejoiceth more of that sheep , than of the ninety and nine which went not astray.
Kigiriki
Καὶ ἐὰν γένηται εὑρεῖν αὐτό, ἀμὴν λέγω ὑμῖν ὅτι χαίρει ἐπ’ αὐτῷ μᾶλλον, ἢ ἐπὶ τοῖς ἐνενήκοντα ἐννέα τοῖς μὴ πεπλανημένοις.
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
Kai ean genētai heurein auto, amēn legō hymin hoti chairei ep’ autō mallon, ē epi tois enenēkonta ennea tois mē peplanēmenois.
MATHAYO 18:14 TWMC · Kiswahili
Vivyo hivyo si mapenzi ya Baba yenu aliye mbinguni kwamba hata mmoja wa hawa wadogo apotee.
KJV · English
Even so it is not the will of your Father which is in heaven, that one of these little ones should perish.
Kigiriki
Οὕτως οὐκ ἔστιν θέλημα ἔμπροσθεν τοῦ πατρὸς ὑμῶν τοῦ ἐν οὐρανοῖς, ἵνα ἀπόληται εἷς τῶν μικρῶν τούτων.
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
Houtōs ouk estin thelēma emprosthen tou patros hymōn tou en ouranois, hina apolētai heis tōn mikrōn toutōn.
MATHAYO 18:15 TWMC · Kiswahili
Ndugu yako akikukosea, nenda ukamwonyeshe kosa lake, wewe naye peke yenu. Akikusikiliza, umempata ndugu yako tena.
KJV · English
¶ Moreover if thy brother shall trespass against thee, go and tell him his fault between thee and him alone: if he shall hear thee, thou hast gained thy brother.
Kigiriki
Ἐὰν δὲ ἁμαρτήσῃ εἰς σὲ ὁ ἀδελφός σου, ὕπαγε καὶ ἔλεγξον αὐτὸν μεταξὺ σοῦ καὶ αὐτοῦ μόνου. Ἐάν σου ἀκούσῃ, ἐκέρδησας τὸν ἀδελφόν σου∙
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
Ean de hamartēsē eis se ho adelphos sou, hypage kai elenxon auton metaxy sou kai autou monou. Ean sou akousē, ekerdēsas ton adelphon sou;
MATHAYO 18:16 TWMC · Kiswahili
Asipokusikiliza, chukua pamoja nawe mtu mmoja au wawili, ili kila jambo lithibitishwe kwa ushahidi wa mashahidi wawili au watatu.
KJV · English
But if he will not hear thee, then take with thee one or two more, that in the mouth of two or three witnesses every word may be established.
Kigiriki
ἐὰν δὲ μὴ ἀκούσῃ, παράλαβε μετὰ σοῦ ἔτι ἕνα ἢ δύο, ἵνα ἐπὶ στόματος δύο μαρτύρων ἢ τριῶν σταθῇ πᾶν ῥῆμα∙
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
ean de mē akousē, paralabe meta sou eti hena ē dyo, hina epi stomatos dyo martyrōn ē triōn stathē pan rhēma;
MATHAYO 18:17 TWMC · Kiswahili
Asipowasikiliza, liambie kanisa. Asipolisikiliza hata kanisa, basi awe kwako kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru.
KJV · English
And if he shall neglect to hear them, tell it unto the church: but if he neglect to hear the church, let him be unto thee as an heathen man and a publican.
Kigiriki
ἐὰν δὲ παρακούσῃ αὐτῶν, εἰπὲ τῇ ἐκκλησίᾳ∙ ἐὰν δὲ καὶ τῆς ἐκκλησίας παρακούσῃ, ἔστω σοι ὥσπερ ὁ ἐθνικὸς καὶ ὁ τελώνης.
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
ean de parakousē autōn, eipe tē ekklēsia; ean de kai tēs ekklēsias parakousē, estō soi hōsper ho ethnikos kai ho telōnēs.
MATHAYO 18:18 TWMC · Kiswahili
Kwa kweli nawaambia, vyote mtakavyofunga duniani vitakuwa vimefungwa mbinguni, na vyote mtakavyofungua duniani vitakuwa vimefunguliwa mbinguni.
KJV · English
Verily I say unto you, Whatsoever ye shall bind on earth shall be bound in heaven: and whatsoever ye shall loose on earth shall be loosed in heaven.
Kigiriki
Ἀμὴν λέγω ὑμῖν, ὅσα ἐὰν δήσητε ἐπὶ τῆς γῆς, ἔσται δεδεμένα ἐν τῷ οὐρανῷ∙ καὶ ὅσα ἐὰν λύσητε ἐπὶ τῆς γῆς, ἔσται λελυμένα ἐν τῷ οὐρανῷ.
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
Amēn legō hymin, hosa ean dēsēte epi tēs gēs, estai dedemena en tō ouranō; kai hosa ean lysēte epi tēs gēs, estai lelymena en tō ouranō.
MATHAYO 18:19 TWMC · Kiswahili
Tena kwa kweli nawaambia, wawili kati yenu duniani wakikubaliana kuhusu jambo lolote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni.
KJV · English
Again I say unto you, That if two of you shall agree on earth as touching any thing that they shall ask, it shall be done for them of my Father which is in heaven.
Kigiriki
Πάλιν ἀμὴν λέγω ὑμῖν ὅτι ἐὰν δύο ὑμῶν συμφωνήσωσιν ἐπὶ τῆς γῆς περὶ παντὸς πράγματος οὗ ἐὰν αἰτήσωνται, γενήσεται αὐτοῖς παρὰ τοῦ πατρός μου τοῦ ἐν οὐρανοῖς.
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
Palin amēn legō hymin hoti ean dyo hymōn symphōnēsōsin epi tēs gēs peri pantos pragmatos hou ean aitēsōntai, genēsetai autois para tou patros mou tou en ouranois.
MATHAYO 18:20 TWMC · Kiswahili
Kwa maana walipo wawili au watatu waliokusanyika kwa jina langu, hapo niko katikati yao.”
KJV · English
For where two or three are gathered together in my name, there am I in the midst of them.
Kigiriki
Οὗ γάρ εἰσιν δύο ἢ τρεῖς συνηγμένοι εἰς τὸ ἐμὸν ὄνομα, ἐκεῖ εἰμὶ ἐν μέσῳ αὐτῶν.
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
Hou gar eisin dyo ē treis synēgmenoi eis to emon onoma, ekei eimi en mesō autōn.
MATHAYO 18:21 TWMC · Kiswahili
Ndipo Petro akamjia Yesu, akamuuliza, “Bwana, ndugu yangu atanikosea mara ngapi nami nimsamehe? Hata mara saba?”
KJV · English
¶ Then came Peter to him, and said, Lord, how oft shall my brother sin against me, and I forgive him? till seven times?
Kigiriki
Τότε προσελθὼν αὐτῷ ὁ Πέτρος εἶπεν, Κύριε, ποσάκις ἁμαρτήσει εἰς ἐμὲ ὁ ἀδελφός μου, καὶ ἀφήσω αὐτῷ; Ἕως ἑπτάκις;
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
Tote proselthōn autō ho Petros eipen, Kyrie, posakis hamartēsei eis eme ho adelphos mou, kai aphēsō autō? Heōs heptakis?
MATHAYO 18:22 TWMC · Kiswahili
Yesu akamwambia, “Sikuambii mpaka mara saba, bali mpaka mara sabini mara saba.
KJV · English
Jesus saith unto him, I say not unto thee, Until seven times: but, Until seventy times seven.
Kigiriki
Λέγει αὐτῷ ὁ Ἰησοῦς, Οὐ λέγω σοι ἕως ἑπτάκις, ἀλλ’ ἕως ἑβδομηκοντάκις ἑπτά.
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
Legei autō ho Iēsous, Ou legō soi heōs heptakis, all’ heōs hebdomēkontakis hepta.
MATHAYO 18:23 TWMC · Kiswahili
Kwa hiyo Ufalme wa mbinguni umefananishwa na mfalme aliyetaka kufanya hesabu na watumishi wake.
KJV · English
¶ Therefore is the kingdom of heaven likened unto a certain king, which would take account of his servants.
Kigiriki
Διὰ τοῦτο ὡμοιώθη ἡ βασιλεία τῶν οὐρανῶν ἀνθρώπῳ βασιλεῖ, ὃς ἠθέλησεν συνᾶραι λόγον μετὰ τῶν δούλων αὐτοῦ.
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
Dia touto hōmoiōthē hē basileia tōn ouranōn anthrōpō basilei, hos ēthelēsen synarai logon meta tōn doulōn autou.
MATHAYO 18:24 TWMC · Kiswahili
Alipoanza kufanya hesabu, akaletewa mmoja aliyekuwa na deni la talanta elfu kumi.
KJV · English
And when he had begun to reckon, one was brought unto him, which owed him ten thousand talents.
Kigiriki
Ἀρξαμένου δὲ αὐτοῦ συναίρειν, προσηνέχθη αὐτῷ εἷς ὀφειλέτης μυρίων ταλάντων.
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
Arxamenou de autou synairein, prosēnechthē autō heis opheiletēs myriōn talantōn.
MATHAYO 18:25 TWMC · Kiswahili
Kwa kuwa hakuwa na cha kulipa, bwana wake akaamuru auzwe, pamoja na mke wake, watoto wake na vyote alivyokuwa navyo, ili deni lilipwe.
KJV · English
But forasmuch as he had not to pay, his lord commanded him to be sold, and his wife, and children, and all that he had, and payment to be made.
Kigiriki
Μὴ ἔχοντος δὲ αὐτοῦ ἀποδοῦναι ἐκέλευσεν αὐτὸν ὁ κύριος αὐτοῦ πραθῆναι, καὶ τὴν γυναῖκα αὐτοῦ καὶ τὰ τέκνα, καὶ πάντα ὅσα εἶχεν, καὶ ἀποδοθῆναι.
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
Mē echontos de autou apodounai ekeleusen auton ho kyrios autou prathēnai, kai tēn gynaika autou kai ta tekna, kai panta hosa eichen, kai apodothēnai.
MATHAYO 18:26 TWMC · Kiswahili
Yule mtumishi akaanguka mbele yake, akamsujudia, akisema, ‘Bwana, nivumilie, nami nitakulipa vyote.’
KJV · English
The servant therefore fell down, and worshipped him, saying, Lord, have patience with me, and I will pay thee all.
Kigiriki
Πεσὼν οὖν ὁ δοῦλος προσεκύνει αὐτῷ, λέγων, Κύριε, μακροθύμησον ἐπ’ ἐμοί, καὶ πάντα σοι ἀποδώσω.
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
Pesōn oun ho doulos prosekynei autō, legōn, Kyrie, makrothymēson ep’ emoi, kai panta soi apodōsō.
MATHAYO 18:27 TWMC · Kiswahili
Bwana wake akamwonea huruma, akamwachilia na kumsamehe deni.
KJV · English
Then the lord of that servant was moved with compassion, and loosed him, and forgave him the debt.
Kigiriki
Σπλαγχνισθεὶς δὲ ὁ κύριος τοῦ δούλου ἐκείνου ἀπέλυσεν αὐτόν, καὶ τὸ δάνειον ἀφῆκεν αὐτῷ.
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
Splanchnistheis de ho kyrios tou doulou ekeinou apelysen auton, kai to daneion aphēken autō.
MATHAYO 18:28 TWMC · Kiswahili
Lakini mtumishi huyo alipotoka, akamkuta mtumishi mwenzake aliyekuwa na deni kwake la denari mia moja. Akamkamata na kumkaba koo,
akisema, ‘Nilipe ninachokudai!’
KJV · English
But the same servant went out, and found one of his fellowservants, which owed him an hundred pence: and he laid hands on him, and took him by the throat, saying, Pay me that thou owest.
Kigiriki
Ἐξελθὼν δὲ ὁ δοῦλος ἐκεῖνος εὗρεν ἕνα τῶν συνδούλων αὐτοῦ, ὃς ὤφειλεν αὐτῷ ἑκατὸν δηνάρια, καὶ κρατήσας αὐτὸν ἔπνιγεν, λέγων, Ἀπόδος μοι εἴ τι ὀφείλεις.
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
Exelthōn de ho doulos ekeinos heuren hena tōn syndoulōn autou, hos ōpheilen autō hekaton dēnaria, kai kratēsas auton epnigen, legōn, Apodos moi ei ti opheileis.
MATHAYO 18:29 TWMC · Kiswahili
Mtumishi mwenzake akaanguka miguuni pake, akamsihi, ‘Nivumilie, nami nitakulipa.’
KJV · English
And his fellowservant fell down at his feet, and besought him, saying, Have patience with me, and I will pay thee all.
Kigiriki
Πεσὼν οὖν ὁ σύνδουλος αὐτοῦ εἰς τοὺς πόδας αὐτοῦ παρεκάλει αὐτόν, λέγων, Μακροθύμησον ἐπ’ ἐμοί, καὶ ἀποδώσω σοι.
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
Pesōn oun ho syndoulos autou eis tous podas autou parekalei auton, legōn, Makrothymēson ep’ emoi, kai apodōsō soi.
MATHAYO 18:30 TWMC · Kiswahili
Lakini hakutaka. Badala yake akaenda kumtia gerezani mpaka alipe deni.
KJV · English
And he would not: but went and cast him into prison, till he should pay the debt.
Kigiriki
Ὁ δὲ οὐκ ἤθελεν, ἀλλὰ ἀπελθὼν ἔβαλεν αὐτὸν εἰς φυλακήν, ἕως οὗ ἀποδῷ τὸ ὀφειλόμενον.
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
Ho de ouk ēthelen, alla apelthōn ebalen auton eis phylakēn, heōs hou apodō to opheilomenon.
MATHAYO 18:31 TWMC · Kiswahili
Watumishi wenzake walipoona yaliyotokea, walihuzunika sana. Wakaenda kumweleza bwana wao yote yaliyotokea.
KJV · English
So when his fellowservants saw what was done, they were very sorry, and came and told unto their lord all that was done.
Kigiriki
Ἰδόντες δὲ οἱ σύνδουλοι αὐτοῦ τὰ γενόμενα ἐλυπήθησαν σφόδρα∙ καὶ ἐλθόντες διεσάφησαν τῷ κυρίῳ ἑαυτῶν πάντα τὰ γενόμενα.
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
Idontes de hoi syndouloi autou ta genomena elypēthēsan sphodra; kai elthontes diesaphēsan tō kyriō heautōn panta ta genomena.
MATHAYO 18:32 TWMC · Kiswahili
Ndipo bwana wake akamwita yule mtumishi,
akamwambia, ‘Mtumishi mwovu! Nilikusamehe deni lile lote kwa sababu ulinisihi.
KJV · English
Then his lord, after that he had called him, said unto him, O thou wicked servant, I forgave thee all that debt, because thou desiredst me:
Kigiriki
Τότε προσκαλεσάμενος αὐτὸν ὁ κύριος αὐτοῦ λέγει αὐτῷ, Δοῦλε πονηρέ, πᾶσαν τὴν ὀφειλὴν ἐκείνην ἀφῆκά σοι, ἐπεὶ παρεκάλεσάς με∙
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
Tote proskalesamenos auton ho kyrios autou legei autō, Doule ponēre, pasan tēn opheilēn ekeinēn aphēka soi, epei parekalesas me;
MATHAYO 18:33 TWMC · Kiswahili
Je, nawe hukupaswa kumhurumia mtumishi mwenzako kama nilivyokuhurumia?’
KJV · English
Shouldest not thou also have had compassion on thy fellowservant, even as I had pity on thee?
Kigiriki
οὐκ ἔδει καὶ σὲ ἐλεῆσαι τὸν σύνδουλόν σου, ὡς καὶ ἐγώ σε ἠλέησα;
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
ouk edei kai se eleēsai ton syndoulon sou, hōs kai egō se ēleēsa?
MATHAYO 18:34 TWMC · Kiswahili
Bwana wake akakasirika, akamkabidhi kwa watesaji mpaka alipe deni lake lote.
KJV · English
And his lord was wroth, and delivered him to the tormentors, till he should pay all that was due unto him.
Kigiriki
Καὶ ὀργισθεὶς ὁ κύριος αὐτοῦ παρέδωκεν αὐτὸν τοῖς βασανισταῖς, ἕως οὗ ἀποδῷ πᾶν τὸ ὀφειλόμενον αὐτῷ.
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
Kai orgistheis ho kyrios autou paredōken auton tois basanistais, heōs hou apodō pan to opheilomenon autō.
MATHAYO 18:35 TWMC · Kiswahili
Ndivyo Baba yangu wa mbinguni atakavyowatendea ninyi, kama kila mmoja wenu hatamsamehe ndugu yake makosa yake kutoka moyoni.”
KJV · English
So likewise shall my heavenly Father do also unto you, if ye from your hearts forgive not every one his brother their trespasses.
Kigiriki
Οὕτως καὶ ὁ πατήρ μου ὁ ἐπουράνιος ποιήσει ὑμῖν, ἐὰν μὴ ἀφῆτε ἕκαστος τῷ ἀδελφῷ αὐτοῦ ἀπὸ τῶν καρδιῶν ὑμῶν τὰ παραπτώματα αὐτῶν.
Kigiriki kwa herufi za Kirumi
Houtōs kai ho patēr mou ho epouranios poiēsei hymin, ean mē aphēte hekastos tō adelphō autou apo tōn kardiōn hymōn ta paraptōmata autōn.