The Word,
Made Clear
Read the Bible free
Kiswahili · Mathayo

Mathayo 8

Nani, nini, kwa nini, lini, wapi na jinsi — utangulizi wa kitabu

Jinsi ya kutumia uchunguzi wa maneno ya Kigiriki

Huhitaji kujua kusoma Kigiriki ili kuanza. Gusa neno lililopigiwa mstari katika mstari wa Kigiriki au wa Kigiriki kilichoandikwa kwa herufi za Kilatini: yote mawili yanafungua ingizo lilelile. Data inapopatikana kwa uhakika, utaona umbo la neno katika kamusi, sarufi, namba ya Strong na maana. Chagua “Zaidi kuhusu maana na sarufi” ili kuona maelezo zaidi. Buruta upau wa juu ili kusogeza paneli, na sogeza yaliyomo ndani yake ili kuendelea kusoma. Kitufe cha “Funga” hubaki kuonekana.

Mstari wa vipande unaonyesha kwamba uchanganuzi haupatikani; mstari maradufu unaonyesha kwamba ingizo la kamusi halipatikani. Hatujazii mapengo haya kwa kubahatisha. Kamusi hutoa maana zinazowezekana; muktadha huamua maana inayofaa katika kifungu. Maandishi yetu ya Biblia, Kigiriki na herufi za Kilatini hayajabadilishwa.

RASIMU KWA UHAKIKI: Maana za kamusi kwa Kiswahili ni tafsiri za kiotomatiki za ufafanuzi wa Kiingereza wa Dodson, pamoja na masahihisho maalumu. Bado zinahitaji uhakiki wa mwandishi na wa lugha. Ufafanuzi wa awali wa Kiingereza unapatikana katika maelezo yaliyopanuliwa. Alama hii ya rasimu inahusu maana za kamusi pekee, si maandishi yaliyokamilika ya Biblia.

Soma kuhusu vyanzo na upeo wa matumizi →
MATHAYO 8:1
TWMC · Kiswahili

Yesu aliposhuka mlimani, makutano makubwa yakamfuata.

KJV · English

When he was come down from the mountain, great multitudes followed him.

Kigiriki

Καταβάντι δὲ αὐτῷ ἀπὸ τοῦ ὄρους, ἠκολούθησαν αὐτῷ ὄχλοι πολλοί∙

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Katabanti de autō apo tou orous, ēkolouthēsan autō ochloi polloi;

MATHAYO 8:2
TWMC · Kiswahili

Tazama, mtu mwenye ukoma akamjia, akasujudu mbele yake na kusema, “Bwana, ukitaka, unaweza kunitakasa.”

KJV · English

And, behold, there came a leper and worshipped him, saying, Lord, if thou wilt, thou canst make me clean.

Kigiriki

καὶ ἰδού, λεπρὸς ἐλθὼν προσεκύνει αὐτῷ, λέγων, Κύριε, ἐὰν θέλῃς, δύνασαί με καθαρίσαι.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

kai idou, lepros elthōn prosekynei autō, legōn, Kyrie, ean thelēs, dynasai me katharisai.

MATHAYO 8:3
TWMC · Kiswahili

Yesu akaunyosha mkono na kumgusa.

“Nataka,” akasema. “Takasika.”

Mara yule mtu akatakasika na ukoma wake ukaondoka.

KJV · English

And Jesus put forth his hand, and touched him, saying, I will; be thou clean. And immediately his leprosy was cleansed.

Kigiriki

Καὶ ἐκτείνας τὴν χεῖρα, ἥψατο αὐτοῦ ὁ Ἰησοῦς, λέγων, Θέλω, καθαρίσθητι. Καὶ εὐθέως ἐκαθαρίσθη αὐτοῦ ἡ λέπρα.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Kai ekteinas tēn cheira, hēpsato autou ho Iēsous, legōn, Thelō, katharisthēti. Kai eutheōs ekatharisthē autou hē lepra.

MATHAYO 8:4
TWMC · Kiswahili

Kisha Yesu akamwambia, “Angalia, usimwambie mtu yeyote. Bali nenda ukajionyeshe kwa kuhani, ukatoe sadaka aliyoamuru Musa, iwe ushuhuda kwao.”

KJV · English

And Jesus saith unto him, See thou tell no man; but go thy way, shew thyself to the priest, and offer the gift that Moses commanded, for a testimony unto them.

Kigiriki

Καὶ λέγει αὐτῷ ὁ Ἰησοῦς, Ὅρα μηδενὶ εἴπῃς∙ ἀλλὰ ὕπαγε, σεαυτὸν δεῖξον τῷ ἱερεῖ, καὶ προσένεγκε τὸ δῶρον ὃ προσέταξεν Μωσῆς, εἰς μαρτύριον αὐτοῖς.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Kai legei autō ho Iēsous, Hora mēdeni eipēs; alla hypage, seauton deixon tō hierei, kai prosenenke to dōron ho prosetaxen Mōsēs, eis martyrion autois.

MATHAYO 8:5
TWMC · Kiswahili

Yesu alipoingia Kapernaumu, mkuu wa kikosi cha askari mia akamjia akimsihi msaada.

KJV · English

¶ And when Jesus was entered into Capernaum, there came unto him a centurion, beseeching him,

Kigiriki

Εἰσελθόντι δὲ αὐτῷ εἰς Καπερναούμ, προσῆλθεν αὐτῷ ἑκατόνταρχος παρακαλῶν αὐτόν,

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Eiselthonti de autō eis Kapernaoum, prosēlthen autō hekatontarchos parakalōn auton,

MATHAYO 8:6
TWMC · Kiswahili

Akasema, “Bwana, mtumishi wangu amelala nyumbani amepooza, akiteseka sana.”

KJV · English

And saying, Lord, my servant lieth at home sick of the palsy, grievously tormented.

Kigiriki

καὶ λέγων, Κύριε, ὁ παῖς μου βέβληται ἐν τῇ οἰκίᾳ παραλυτικός, δεινῶς βασανιζόμενος.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

kai legōn, Kyrie, ho pais mou beblētai en tē oikia paralytikos, deinōs basanizomenos.

MATHAYO 8:7
TWMC · Kiswahili

Yesu akamwambia, “Nitakuja kumponya.”

KJV · English

And Jesus saith unto him, I will come and heal him.

Kigiriki

Καὶ λέγει αὐτῷ ὁ Ἰησοῦς, Ἐγὼ ἐλθὼν θεραπεύσω αὐτόν.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Kai legei autō ho Iēsous, Egō elthōn therapeusō auton.

MATHAYO 8:8
TWMC · Kiswahili

Lakini yule mkuu wa kikosi akajibu, “Bwana, sistahili wewe kuingia chini ya paa langu. Sema neno tu, na mtumishi wangu atapona.

KJV · English

The centurion answered and said, Lord, I am not worthy that thou shouldest come under my roof: but speak the word only, and my servant shall be healed.

Kigiriki

Καὶ ἀποκριθεὶς ὁ ἑκατόνταρχος ἔφη, Κύριε, οὐκ εἰμὶ ἱκανὸς ἵνα μου ὑπὸ τὴν στέγην εἰσέλθῃς∙ ἀλλὰ μόνον εἰπὲ λόγῳ, καὶ ἰαθήσεται ὁ παῖς μου.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Kai apokritheis ho hekatontarchos ephē, Kyrie, ouk eimi hikanos hina mou hypo tēn stegēn eiselthēs; alla monon eipe logō, kai iathēsetai ho pais mou.

MATHAYO 8:9
TWMC · Kiswahili

Kwa maana mimi pia ni mtu aliye chini ya mamlaka, nami nina askari chini yangu. Nikimwambia mmoja, ‘Nenda,’ huenda; mwingine, ‘Njoo,’ huja. Nikimwambia mtumishi wangu, ‘Fanya hivi,’ hufanya.”

KJV · English

For I am a man under authority, having soldiers under me: and I say to this man, Go, and he goeth; and to another, Come, and he cometh; and to my servant, Do this, and he doeth it.

Kigiriki

Καὶ γὰρ ἐγὼ ἄνθρωπός εἰμι ὑπὸ ἐξουσίαν, ἔχων ὑπ’ ἐμαυτὸν στρατιώτας∙ καὶ λέγω τούτῳ, Πορεύθητι, καὶ πορεύεται∙ καὶ ἄλλῳ, Ἔρχου, καὶ ἔρχεται∙ καὶ τῷ δούλῳ μου, Ποίησον τοῦτο, καὶ ποιεῖ.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Kai gar egō anthrōpos eimi hypo exousian, echōn hyp’ emauton stratiōtas; kai legō toutō, Poreuthēti, kai poreuetai; kai allō, Erchou, kai erchetai; kai tō doulō mou, Poiēson touto, kai poiei.

MATHAYO 8:10
TWMC · Kiswahili

Yesu aliposikia hayo, alishangaa. Akawaambia waliokuwa wakimfuata, “Kwa kweli nawaambia: hata katika Israeli sijaona imani kubwa namna hii.

KJV · English

When Jesus heard it, he marvelled, and said to them that followed, Verily I say unto you, I have not found so great faith, no, not in Israel.

Kigiriki

Ἀκούσας δὲ ὁ Ἰησοῦς ἐθαύμασεν, καὶ εἶπεν τοῖς ἀκολουθοῦσιν, Ἀμὴν λέγω ὑμῖν, οὐδὲ ἐν τῷ Ἰσραὴλ τοσαύτην πίστιν εὗρον.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Akousas de ho Iēsous ethaumasen, kai eipen tois akolouthousin, Amēn legō hymin, oude en tō Israēl tosautēn pistin heuron.

MATHAYO 8:11
TWMC · Kiswahili

Nawaambia kwamba wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, nao wataketi mezani pamoja na Abrahamu, Isaka, na Yakobo katika Ufalme wa mbinguni.

KJV · English

And I say unto you, That many shall come from the east and west, and shall sit down with Abraham, and Isaac, and Jacob, in the kingdom of heaven.

Kigiriki

Λέγω δὲ ὑμῖν ὅτι πολλοὶ ἀπὸ ἀνατολῶν καὶ δυσμῶν ἥξουσιν, καὶ ἀνακλιθήσονται μετὰ Ἀβραὰμ καὶ Ἰσαὰκ καὶ Ἰακὼβ ἐν τῇ βασιλείᾳ τῶν οὐρανῶν∙

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Legō de hymin hoti polloi apo anatolōn kai dysmōn hēxousin, kai anaklithēsontai meta Abraam kai Isaak kai Iakōb en tē basileia tōn ouranōn;

MATHAYO 8:12
TWMC · Kiswahili

Lakini wana wa Ufalme watatupwa nje gizani. Huko kutakuwa na kilio na kusaga meno.”

KJV · English

But the children of the kingdom shall be cast out into outer darkness: there shall be weeping and gnashing of teeth.

Kigiriki

οἱ δὲ υἱοὶ τῆς βασιλείας ἐκβληθήσονται εἰς τὸ σκότος τὸ ἐξώτερον∙ ἐκεῖ ἔσται ὁ κλαυθμὸς καὶ ὁ βρυγμὸς τῶν ὀδόντων.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

hoi de huioi tēs basileias ekblēthēsontai eis to skotos to exōteron; ekei estai ho klauthmos kai ho brygmos tōn odontōn.

MATHAYO 8:13
TWMC · Kiswahili

Kisha Yesu akamwambia mkuu wa kikosi, “Nenda; na iwe kwako kama ulivyoamini.”

Naye mtumishi wake akapona saa ileile.

KJV · English

And Jesus said unto the centurion, Go thy way; and as thou hast believed, so be it done unto thee. And his servant was healed in the selfsame hour.

Kigiriki

Καὶ εἶπεν ὁ Ἰησοῦς τῷ ἑκατοντάρχῃ, Ὕπαγε, καὶ ὡς ἐπίστευσας γενηθήτω σοι. Καὶ ἰάθη ὁ παῖς αὐτοῦ ἐν τῇ ὥρᾳ ἐκείνῃ.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Kai eipen ho Iēsous tō hekatontarchē, Hypage, kai hōs episteusas genēthētō soi. Kai iathē ho pais autou en tē hōra ekeinē.

MATHAYO 8:14
TWMC · Kiswahili

Yesu alipoingia nyumbani kwa Petro, alimwona mama mkwe wa Petro amelala, akiwa na homa.

KJV · English

¶ And when Jesus was come into Peter’s house, he saw his wife’s mother laid, and sick of a fever.

Kigiriki

Καὶ ἐλθὼν ὁ Ἰησοῦς εἰς τὴν οἰκίαν Πέτρου, εἶδεν τὴν πενθερὰν αὐτοῦ βεβλημένην καὶ πυρέσσουσαν,

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Kai elthōn ho Iēsous eis tēn oikian Petrou, eiden tēn pentheran autou beblēmenēn kai pyressousan,

MATHAYO 8:15
TWMC · Kiswahili

Yesu akamgusa mkono, homa ikamwacha. Akaamka na kuanza kumhudumia.

KJV · English

And he touched her hand, and the fever left her: and she arose, and ministered unto them.

Kigiriki

καὶ ἥψατο τῆς χειρὸς αὐτῆς, καὶ ἀφῆκεν αὐτὴν ὁ πυρετός∙ καὶ ἠγέρθη, καὶ διηκόνει αὐτῷ.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

kai hēpsato tēs cheiros autēs, kai aphēken autēn ho pyretos; kai ēgerthē, kai diēkonei autō.

MATHAYO 8:16
TWMC · Kiswahili

Jioni ilipofika, watu wakamletea wengi waliokuwa na pepo. Akawafukuza wale roho kwa neno, na kuwaponya wote waliokuwa wagonjwa.

KJV · English

¶ When the even was come, they brought unto him many that were possessed with devils: and he cast out the spirits with his word, and healed all that were sick:

Kigiriki

Ὀψίας δὲ γενομένης προσήνεγκαν αὐτῷ δαιμονιζομένους πολλούς∙ καὶ ἐξέβαλεν τὰ πνεύματα λόγῳ, καὶ πάντας τοὺς κακῶς ἔχοντας ἐθεράπευσεν∙

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Opsias de genomenēs prosēnenkan autō daimonizomenous pollous; kai exebalen ta pneumata logō, kai pantas tous kakōs echontas etherapeusen;

MATHAYO 8:17
TWMC · Kiswahili

Hivyo yakatimia yaliyosemwa kupitia nabii Isaya:

“Yeye alichukua udhaifu wetu,

na kubeba magonjwa yetu.”

KJV · English

That it might be fulfilled which was spoken by Esaias the prophet, saying, Himself took our infirmities, and bare our sicknesses.

Kigiriki

ὅπως πληρωθῇ τὸ ῥηθὲν διὰ Ἠσαΐου τοῦ προφήτου, λέγοντος, Αὐτὸς τὰς ἀσθενείας ἡμῶν ἔλαβεν, καὶ τὰς νόσους ἐβάστασεν.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

hopōs plērōthē to rhēthen dia Ēsaiou tou prophētou, legontos, Autos tas astheneias hēmōn elaben, kai tas nosous ebastasen.

MATHAYO 8:18
TWMC · Kiswahili

Yesu alipoona makutano makubwa yakimzunguka, aliamuru wavuke kwenda ng'ambo ya ziwa.

KJV · English

¶ Now when Jesus saw great multitudes about him, he gave commandment to depart unto the other side.

Kigiriki

Ἰδὼν δὲ ὁ Ἰησοῦς πολλοὺς ὄχλους περὶ αὐτόν, ἐκέλευσεν ἀπελθεῖν εἰς τὸ πέραν.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Idōn de ho Iēsous pollous ochlous peri auton, ekeleusen apelthein eis to peran.

MATHAYO 8:19
TWMC · Kiswahili

Mwandishi mmoja wa sheria akamjia akasema, “Mwalimu, nitakufuata popote utakapoenda.”

KJV · English

And a certain scribe came, and said unto him, Master, I will follow thee whithersoever thou goest.

Kigiriki

Καὶ προσελθὼν εἷς γραμματεὺς εἶπεν αὐτῷ, Διδάσκαλε, ἀκολουθήσω σοι ὅπου ἐὰν ἀπέρχῃ.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Kai proselthōn heis grammateus eipen autō, Didaskale, akolouthēsō soi hopou ean aperchē.

MATHAYO 8:20
TWMC · Kiswahili

Yesu akamjibu, “Mbweha wana mapango, na ndege wa angani wana viota, lakini Mwana wa Adamu hana mahali pa kulaza kichwa chake.”

KJV · English

And Jesus saith unto him, The foxes have holes, and the birds of the air have nests; but the Son of man hath not where to lay his head.

Kigiriki

Καὶ λέγει αὐτῷ ὁ Ἰησοῦς, Αἱ ἀλώπεκες φωλεοὺς ἔχουσιν, καὶ τὰ πετεινὰ τοῦ οὐρανοῦ κατασκηνώσεις∙ ὁ δὲ υἱὸς τοῦ ἀνθρώπου οὐκ ἔχει ποῦ τὴν κεφαλὴν κλίνῃ.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Kai legei autō ho Iēsous, Hai alōpekes phōleous echousin, kai ta peteina tou ouranou kataskēnōseis; ho de huios tou anthrōpou ouk echei pou tēn kephalēn klinē.

MATHAYO 8:21
TWMC · Kiswahili

Mwingine wa wanafunzi wake akamwambia, “Bwana, niruhusu kwanza niende kumzika baba yangu.”

KJV · English

And another of his disciples said unto him, Lord, suffer me first to go and bury my father.

Kigiriki

Ἕτερος δὲ τῶν μαθητῶν αὐτοῦ εἶπεν αὐτῷ, Κύριε, ἐπίτρεψόν μοι πρῶτον ἀπελθεῖν καὶ θάψαι τὸν πατέρα μου.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Heteros de tōn mathētōn autou eipen autō, Kyrie, epitrepson moi prōton apelthein kai thapsai ton patera mou.

MATHAYO 8:22
TWMC · Kiswahili

Lakini Yesu akamwambia, “Nifuate, na uwaache wafu wawazike wafu wao wenyewe.”

KJV · English

But Jesus said unto him, Follow me; and let the dead bury their dead.

Kigiriki

Ὁ δὲ Ἰησοῦς εἶπεν αὐτῷ, Ἀκολούθει μοι, καὶ ἄφες τοὺς νεκροὺς θάψαι τοὺς ἑαυτῶν νεκρούς.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Ho de Iēsous eipen autō, Akolouthei moi, kai aphes tous nekrous thapsai tous heautōn nekrous.

MATHAYO 8:23
TWMC · Kiswahili

Yesu akaingia mashuani, na wanafunzi wake wakamfuata.

KJV · English

¶ And when he was entered into a ship, his disciples followed him.

Kigiriki

Καὶ ἐμβάντι αὐτῷ εἰς τὸ πλοῖον, ἠκολούθησαν αὐτῷ οἱ μαθηταὶ αὐτοῦ.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Kai embanti autō eis to ploion, ēkolouthēsan autō hoi mathētai autou.

MATHAYO 8:24
TWMC · Kiswahili

Ghafla dhoruba kali ikatokea ziwani, hata mawimbi yakaifunika mashua. Lakini Yesu alikuwa amelala.

KJV · English

And, behold, there arose a great tempest in the sea, insomuch that the ship was covered with the waves: but he was asleep.

Kigiriki

Καὶ ἰδού, σεισμὸς μέγας ἐγένετο ἐν τῇ θαλάσσῃ, ὥστε τὸ πλοῖον καλύπτεσθαι ὑπὸ τῶν κυμάτων∙ αὐτὸς δὲ ἐκάθευδεν.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Kai idou, seismos megas egeneto en tē thalassē, hōste to ploion kalyptesthai hypo tōn kymatōn; autos de ekatheuden.

MATHAYO 8:25
TWMC · Kiswahili

Wanafunzi wake wakamjia wakamwamsha, wakisema:

“Bwana, tuokoe! Tunaangamia!”

KJV · English

And his disciples came to him, and awoke him, saying, Lord, save us: we perish.

Kigiriki

Καὶ προσελθόντες οἱ μαθηταὶ ἤγειραν αὐτόν, λέγοντες, Κύριε, σῶσον ἡμᾶς, ἀπολλύμεθα.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Kai proselthontes hoi mathētai ēgeiran auton, legontes, Kyrie, sōson hēmas, apollymetha.

MATHAYO 8:26
TWMC · Kiswahili

Yesu akawaambia, “Kwa nini mnaogopa, enyi wenye imani haba?”

Kisha akaamka, akaukemea upepo na ziwa, pakawa shwari kabisa.

KJV · English

And he saith unto them, Why are ye fearful, O ye of little faith? Then he arose, and rebuked the winds and the sea; and there was a great calm.

Kigiriki

Καὶ λέγει αὐτοῖς, Τί δειλοί ἐστε, ὀλιγόπιστοι; Τότε ἐγερθεὶς ἐπετίμησεν τοῖς ἀνέμοις καὶ τῇ θαλάσσῃ, καὶ ἐγένετο γαλήνη μεγάλη.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Kai legei autois, Ti deiloi este, oligopistoi? Tote egertheis epetimēsen tois anemois kai tē thalassē, kai egeneto galēnē megalē.

MATHAYO 8:27
TWMC · Kiswahili

Wale watu wakashangaa.

Wakasema, “Huyu ni mtu wa namna gani, hata upepo na ziwa vinamtii?”

KJV · English

But the men marvelled, saying, What manner of man is this, that even the winds and the sea obey him!

Kigiriki

Οἱ δὲ ἄνθρωποι ἐθαύμασαν, λέγοντες, Ποταπός ἐστιν οὗτος, ὅτι καὶ οἱ ἄνεμοι καὶ ἡ θάλασσα ὑπακούουσιν αὐτῷ;

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Hoi de anthrōpoi ethaumasan, legontes, Potapos estin houtos, hoti kai hoi anemoi kai hē thalassa hypakouousin autō?

MATHAYO 8:28
TWMC · Kiswahili

Yesu alipofika ng'ambo, katika eneo la Wagergesi, watu wawili wenye pepo wakamjia kutoka makaburini. Walikuwa wakali sana, hata hakuna aliyeweza kupita njia ile.

KJV · English

¶ And when he was come to the other side into the country of the Gergesenes, there met him two possessed with devils, coming out of the tombs, exceeding fierce, so that no man might pass by that way.

Kigiriki

Καὶ ἐλθόντι αὐτῷ εἰς τὸ πέραν εἰς τὴν χώραν τῶν Γεργεσηνῶν, ὑπήντησαν αὐτῷ δύο δαιμονιζόμενοι ἐκ τῶν μνημείων ἐξερχόμενοι, χαλεποὶ λίαν, ὥστε μὴ ἰσχύειν τινὰ παρελθεῖν διὰ τῆς ὁδοῦ ἐκείνης∙

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Kai elthonti autō eis to peran eis tēn chōran tōn Gergesēnōn, hypēntēsan autō dyo daimonizomenoi ek tōn mnēmeiōn exerchomenoi, chalepoi lian, hōste mē ischyein tina parelthein dia tēs hodou ekeinēs;

MATHAYO 8:29
TWMC · Kiswahili

Ghafla wakapiga kelele, “Una nini nasi, Yesu, Mwana wa Mungu? Je, umekuja hapa kututesa kabla ya wakati uliowekwa?”

KJV · English

And, behold, they cried out, saying, What have we to do with thee, Jesus, thou Son of God? art thou come hither to torment us before the time?

Kigiriki

καὶ ἰδού, ἔκραξαν λέγοντες, Τί ἡμῖν καὶ σοί, Ἰησοῦ υἱὲ τοῦ θεοῦ; Ἦλθες ὧδε πρὸ καιροῦ βασανίσαι ἡμᾶς;

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

kai idou, ekraxan legontes, Ti hēmin kai soi, Iēsou huie tou theou? Ēlthes hōde pro kairou basanisai hēmas?

MATHAYO 8:30
TWMC · Kiswahili

Mbali nao kulikuwa na kundi kubwa la nguruwe likilisha.

KJV · English

And there was a good way off from them an herd of many swine feeding.

Kigiriki

Ἦν δὲ μακρὰν ἀπ’ αὐτῶν ἀγέλη χοίρων πολλῶν βοσκομένη.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Ēn de makran ap’ autōn agelē choirōn pollōn boskomenē.

MATHAYO 8:31
TWMC · Kiswahili

Pepo wakamsihi Yesu, “Ukitufukuza, turuhusu kwenda katika kundi lile la nguruwe.”

KJV · English

So the devils besought him, saying, If thou cast us out, suffer us to go away into the herd of swine.

Kigiriki

Οἱ δὲ δαίμονες παρεκάλουν αὐτόν, λέγοντες, Εἰ ἐκβάλλεις ἡμᾶς, ἐπίτρεψον ἡμῖν ἀπελθεῖν εἰς τὴν ἀγέλην τῶν χοίρων.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Hoi de daimones parekaloun auton, legontes, Ei ekballeis hēmas, epitrepson hēmin apelthein eis tēn agelēn tōn choirōn.

MATHAYO 8:32
TWMC · Kiswahili

Yesu akawaambia, “Nendeni.”

Wakatoka, wakaingia katika kundi la nguruwe. Ghafla kundi lote likakimbia kwa kasi chini ya mteremko mkali mpaka ziwani, likafa majini.

KJV · English

And he said unto them, Go. And when they were come out, they went into the herd of swine: and, behold, the whole herd of swine ran violently down a steep place into the sea, and perished in the waters.

Kigiriki

Καὶ εἶπεν αὐτοῖς, Ὑπάγετε. Οἱ δὲ ἐξελθόντες ἀπῆλθον εἰς τὴν ἀγέλην τῶν χοίρων∙ καὶ ἰδού, ὥρμησεν πᾶσα ἡ ἀγέλη τῶν χοίρων κατὰ τοῦ κρημνοῦ εἰς τὴν θάλασσαν, καὶ ἀπέθανον ἐν τοῖς ὕδασιν.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Kai eipen autois, Hypagete. Hoi de exelthontes apēlthon eis tēn agelēn tōn choirōn; kai idou, hōrmēsen pasa hē agelē tōn choirōn kata tou krēmnou eis tēn thalassan, kai apethanon en tois hydasin.

MATHAYO 8:33
TWMC · Kiswahili

Wachungaji wa nguruwe wakakimbia. Walipofika mjini, wakasimulia kila kitu kilichotokea, pamoja na yaliyowapata wale watu wenye pepo.

KJV · English

And they that kept them fled, and went their ways into the city, and told every thing, and what was befallen to the possessed of the devils.

Kigiriki

Οἱ δὲ βόσκοντες ἔφυγον, καὶ ἀπελθόντες εἰς τὴν πόλιν ἀπήγγειλαν πάντα, καὶ τὰ τῶν δαιμονιζομένων.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Hoi de boskontes ephygon, kai apelthontes eis tēn polin apēngeilan panta, kai ta tōn daimonizomenōn.

MATHAYO 8:34
TWMC · Kiswahili

Basi watu wa mji mzima wakatoka kwenda kukutana na Yesu. Walipomwona, wakamsihi aondoke katika eneo lao.

KJV · English

And, behold, the whole city came out to meet Jesus: and when they saw him, they besought him that he would depart out of their coasts.

Kigiriki

Καὶ ἰδού, πᾶσα ἡ πόλις ἐξῆλθεν εἰς συνάντησιν τῷ Ἰησοῦ∙ καὶ ἰδόντες αὐτόν, παρεκάλεσαν ὅπως μεταβῇ ἀπὸ τῶν ὁρίων αὐτῶν.

Kigiriki kwa herufi za Kirumi

Kai idou, pasa hē polis exēlthen eis synantēsin tō Iēsou; kai idontes auton, parekalesan hopōs metabē apo tōn horiōn autōn.